2014-12-24 15:19:03

Utajiri wa Neno la Mungu


Tabia ya kusherehekea misa tatu na masomo yake – ina maana yake. Kesha: huadhimisha kuzaliwa kwa Bwana na mwokozi – kabla ya nyota nilikuzaa – toka tumbo la Baba. Ni kutangaza Bwana amezaliwa. Wale waliomngoja Bwana katika majilio na wale wanaomsubiri kama mamajusi wanasikia sauti hiyo.

Sherehe iliyojulikana ya kwanza mwaka 336 –baada ya miaka 100 – wakristo wote karibu walirithi tabia hii – chanzo maandiko matakatifu – angalia Injili ya leo. Kwa kuja kwake wakovu umekuja duniani.

Isaya anatupa picha ya mwana mfalme anayezaliwa. Tangu hapo – Isaya anaona uzao huo = ushindi wa Mungu dhidi ya adui zake. Hali hii haikutokea wakati wa uhai wake –sifa juu ya mtoto huyu - amani na haki ya milele - inatuonyesha wazi kuwa Yesu ndiye huyo mwana. Hakika ndiye huyu mshauri wa ajabu, Mungu mkuu, Mungu daima, Mfalme wa amani. Hek. 18:14-15 – ukimya mzito kabisa ulipotanda na usiku mnene – Neno liliingia katikati ya nchi.

Mwinjili Luka anatushikisha utabiri huo wa nabii Isaya. Aidha kadiri ya Isaya mtoto huyu angeonekana – kuja kwa kishindo. Katika Injili ya Luka - siyo. Alizaliwa katika hori- pango. Hakika siyo rahisi kuamini ukuu wake. Luka alikuwa na imani hiyo–tangazo la malaika kwamba huyo ni masiha na Bwana na nyimbo – utukufu kwa Mungu juu …… unakamilisha imani hiyo. Ile iliyokuwa siri - sasa imefunuliwa kwetu. Mwinjili anatambua kuwa katika udogo huo – huyu atakuwa mfalme wa ulimwengu.

Katika Tito – Neema ya Mungu imeonekana kwetu ambapo wokovu unawafikia watu wote.
Katika Efe. 1:5 – toka mwanzo aliazimia kutufanya watoto wake kwa ajili ya Yesu Kristo.
Efe. 1:9 – ametujulisha fumbo la mapenzi yake kadiri ya azimio lake Bwana alilokusudia katika yeye.

Tito 3:4 – uwezo wa upendo kupindua mambo – kipengele mhuri wa tumaini la kikristo –lakini wema wa mwokoziwetu Mungu, na hisani yake kwa wanadamu zilipotokea, ametuokoa – si kwa matendo yetu ….isipokuwa kwa huruma yake.

Hivyo Noeli – ni ufunuo wa juu kabisa wa Mungu – upendo wake kwa wanadamu – mapenzi ya Mungu na upendo wake kwa wanadamu vyaonekana wazi – Tito 3:4.
Sisi tunaalikwa kuishi mapenzi hayo na upendo huo hapa duniani. Wajibu wetu ni kueneza mapendo na haki, kuachana na kila aina ya ubaya na uovu.

Angalisho: wale waliopata taarifa wa kwanza wachungaji waliofunga safari – mamajusi –wanatuambia nini leo katika maisha yetu ya ufuasi/imani? Tunapoadhimisha Noeli tena leo? Ni moyo mnyenyekevu tu unaoweza kutambua na kupokea mambo haya –angalia wachungaji wanasikia malaika wakiimba – utukufu kwa Mungu juu – ni nani hao wenye mapenzi mema?

Mungu amejifanya mtu ili tuweze kumwona – vinginevyo Mungu wetu angebaki mbali – wa kusikika sikika tu. Akajifanya mtu, akawa mtoto – ili sisi tumkaribie Mungu –chombo cha amani na upatanisho. Nasi leo tuna furaha kuimba pamoja na mwinjili Luka 2:14 – utukufu kwa Mungu juu katika maisha yetu.


Asubuhi ya Noeli

Isa. 62:11-12, Tito. 3:4-7, Lk. 2:15-20
Misa yatangaza mwanga wa ulimwengu – kuzaliwa toka tumbo la Maria. Kanisa laadhimisha mapambazuko ya matumaini mapya ya mwanadamu. Mwanzo mpya. Tunaona furaha ya Isaya, ya Tito – maisha ya milele, ya wachungaji. Watu wa kawaida wanaonekana katika pango alipozaliwa Yesu.

Somo la Isaya – lazungumzia ujio wa mwokozi mwishoni mwa utumwa wa Babeli. Wamejitoa katika utumwa – wanaitwa watakatifu – tofauti na watu wa mataifa – wanarudia hali yao ya zamani – watoto wa Mungu. Hata hivyo – Isaya anazungumzia ukombozi ulio zaidi ya mwili = unabii huu – unakamilika katika sherehe hii ya leo – ukombozi wa kweli toka kwa mtoto aliyezaliwa leo.

Wachungaji wanaenda kutangaza habari hiyo njema – mwokozi amezaliwa Habari hii njema – iko wazi katika somo la pili - Yesu ndiye huyo mwokozi. Yuko kati yetu. Mkristo aliyejaa Roho Mtakatifu– anabatizwa katika mwili wa Kristo – Kanisa – na anaendelea kutangaza habari hiyo njema - 1 Pt. 2:9-10. Uwepo wa Kristo = mapambazuko kwetu sisi – wokovu na ubatizo na Roho Mtakatifu – Ef. 5,26.

Hivyo Habari Njema ndiyo hii, Bwana amezaliwa kati yetu. Upendo na uzuri wa Mungu = Kristo. Tito – Kristo – zawadi ya Mungu kwetu - siyo siri tena. Mungu amejifanya mtu akakaa kati yetu – Mt. 1,23. Hiyo zawadi – sisi tunakuwa warithi na uzima wa milele. Mapambazuko haya ya matumaini yanashangaza. Isaya anamtumaini Mungu, Maria anayeweka katika moyo wake, wa wachungaji wanatangaza habari hiyo njema – utukufu wa Mungu.

Kila mkristo asubuhi hii anaushangaa ukuu wa upendo wa Mungu na kuutukuza mpango wake wa ukombozi na jinsi alivyoukamilisha kwa ajili yetu. Tendo hili takatifu linatuwajibisha sote. Tunafanya nini katika ulimwengu wetu wa leo? Mungu amechukua mwili ili sisi tuweze kumwona Mungu kwa macho na kushangaa mambo hayo makuu.


Ibada ya Misa Takatifu wakati wa mchana!

Isa. 52:7-10, Ebr.1:1-6, Yoh.1:1-18
NENO AKATWAA MWILI, AKAKAA KWETU.
Misa ya mchana – husherehekea kuzaliwa kwa Kristo katika mioyo na maisha ya waamini. Sote twajua wazi kuwa hakuna sheria wala falsafa iwezayo kumwokoa mwanadamu. Wokovu wa kweli uko kwa Mungu aliyejifunua kwa njia ya Kristo, yeye ndiye wokovu wetu.

Tuliyoona katika misa ya kesha, usiku, alfajiri na sasa katika misa hii – tukio la Yesu kujifanya mtu – sambamba na tendo la uumbaji – hapo mwanzo: Mwa 1,1. Tofauti hapo, hapo mwanzo ya Yohani iko nje ya wakati. Yohani anasisitiza utukufu wa Kristo. Neno alikuwa Mungu – wengi walitilia mashaka – angalia kina Tomaso baada ya kuushuhudia utukufu huo 20, 28 – Bwana wangu na Mungu wangu -kinachofuata toka kwetu ni wajibu wetu, ushuhuda, kuishi ukweli, haja ya mwanga, haya ya imani.

Huyu Neno amechukua mwili na akaonekana kwetu katika mwili sawa na wa kwetu. Ana hali ya kimungu na ya kibinadamu. Kwa njia yake tunapata nafasi ya kushiriki uzima wa Kimungu. Dunia– haimjui Mungu – kadiri ya Yohani – ingawa kwa njia yake ulimwengu uliumbwa. Yohana aliandaa njia, kwa ufunuo wa mwana wa Mungu - yeye anayetoa neema na ukweli.

Yohana anakuwa mdogo – pia hapa malaika ni wadogo kwake Kristo. Yohani aliandaa njia –kama ilivyo katika somo la kwanza aliongea juu ya mfalme wa haki na amani, raha na wokovu utimilifu huu – Kristo alichukua mwili. Maandalizi ya furaha hii yamefanywa katika Ebrania – anazungumzia juu ya wajibu wa mwana wa Mungu na uhusiano wake na mpango wa ukombozi – juu ya uana wa Mungu, ukuhani wa Yesu na utukufu wa Bwana Yesu mfalme - hapa neno aliyefanywa mtu ni pekee.

Hivi sasa Mungu anaongea nasi kwa njia ya mwanae – si kwa njia ya manabii tena. Yeye ni utimilifu wa dahari. Huyu mwana ndiye sababu ya uwepo wa ulimwengu. Ndiye utukufu wa Mungu Baba. Yesu ni mfano unaonekana wa Mungu asiyeonekana. Anionaye mimi amemwona Baba – Yoh. 12:45. Kwa kuchukua kwake mwili, sisi tumepata nafasi ya kumwona Mungu kwa macho yetu na hali zetu. Ni fumbo ambalo tunaalikwa sana kuendelea kulitafakari ili pole pole aendelea kujifunua kwetu kadiri tunavyoendelea kuungana naye.

Ebr. 2,14 – Yesu ni Mungu, ni mwana wa Mungu, ni Mungu, ni mtu. Noeli – sherehe ya pekee na ya fumbo la pekee - Mungu amezaliwa kwetu – ni juu ya Noeli – sherehe ya pekee na ya fumbo la pekee – Mungu amezaliwa kwetu – ni juu ya yote, ndiye ukamilifu wa yote – aliyetangazwa na Isaya, akatangazwa na Yohani Mbatizaji na akazaliwa kwetu. Anashiriki ubindadamu wetu. Anakuja kwetu na analeta ukombozi. Lengo ni kuunganisha watu wote katika jamii moja. Kwa fumbo hili tunaruka hatua mbele katika ukombozi wetu. Tunamkaribia Mungu. Matumaini yanafunguka na milango ya mbingu inafunguliwa.

Papa leo Mkuu anasema - mtu afurahi kwa kuwa anaikaribia taji ya ushindi. Mtu mwenye dhambi yeye naye afurahi kwa kuwa anasamehewa dhambi zake na mpagani sharti afurahi kwa kuwa anaitwa kupewa uzima.

Na Padre Reginald Mrosso, C.PP.S.








All the contents on this site are copyrighted ©.