Tambua, sasa Yesu yupo, anabisha hodi mlangoni mwa moyo wako
(Vatican Radio) Jumapili, Papa Francisko alitoa mwaliko kwa waamini na wengine wote,
kusikiliza kwa makini sauti ya Mungu anayebisha hodi malangoni mwao. Papa alisema
kwa mara nyingi , Yesu hupita katika maisha yetu, kutupatia ujumbe wa wokovu, lakini
bahati mbaya sisi binadamu huwa tumezingirwa na mawazo mengi, na hivyo tunakosa nafasi
ya kutafakari na kutambua taarifa ya malaika.
Baba Mtakatifu Francisko alitoa
mwaliko huo wakati akizungumza na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa
Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya Sala ya Malaika wa Bwana. Maelezo ya Papa,
yalielekea katika yalijitokeza kwenye Liturujia ya Jumapili ya mwisho ya ujio, inayoeleza
juu ya Malaika Mkuu Gabriel kumtokea Maria na kumtaarifu kuwa atapata mimba kwa uwezo
wa Roho Mtakatifu na atamzaa masiye. Papa alieleza na kuonyesha kushangazwa na jinsi
Maria alivyopokea ujumbe huu kwa unyenyekevu. Maria alisema "ndiyo". Alisema "Mimi
ni mtumishi wa Bwana. Na ifanyike kwangu kama ulivyosema "(Luka 1, 38).
Papa Francis aliendelea kustajabia imani ya Maria ambaye hakujua kitakacho endelea
, iwapo atapambana na uchungu mwingi au kuhatarisha maisha yake, lakini alishika
jambo moja tu kwamba, Bwana amemtaka afanye jambo fulani , na yeye alilikubali kwa
moyo mkunjufu, na matumaini makubwa. Maria alikuwa na imani kubwa! Papa alitaja
kipengele kingine cha kuchukua kama kumbukumbu kwa Maria , ni uwezo wa Maria katika
kuutambua “wakati wa Mungu". Katika tukio hili, alisema, Maria anatufundisha kutambua
wakati mazuri ambamo Yesu hupita katika maisha yetu , akiomba tuwe tayari kutoa jibu
la ukarimu.
Katika wakati huu wa Noeli, Papa aliendelea, Yesu anapita
katika maisha yetu. Wakati wa Krismasi, Yesu yupo anabisha hodi katika moyo wa kila
Mkristo na kila binadamu, akiitwa kujibu, kama Maria, kutoka jibu la kweli binafsi
, kusema "ndiyo", na kujiweka wenyewe katika uwepo wa Mungu na huruma yake. Lakini
Papa alionya , dhidi ya kukosa utambuzi huo, kutokana na hali ya kumezwa na mawazo
kwa mambo ya kidunia, hata katika siku hizi za maandalizi ya Siku Kuu ya Krismasi.
Kuna viashiria vingi lakini watu hawatambui kwamba, kama ni Bwana anayegonga hodi
katika mioyo yetu, akisubiri kukaribishwa .
Baba Mtakatifu aliendelea kuonya
umati dhidi ya watu kumezwa na mambo yao wenyewe , hata katika kipindi hiki cha
maandalizi ya siku kuu ya Noeli. Kukosa hata utambuzi kwamba, ni wakati ambamo Bwana
anagonga hodi katika milango ya mioyo, akiomba kukaribishwa ndani , akisubiri jibu
la ndiyo.
Papa alirejea maneno ya Mtakatifu mmoja aliyesema , “Nina hofia
kumkosa Bwana atakapo pita kwangu” Papa aliitaja hofu hii kuwa ni hofu ya kweli ,
yenye kutatambua uwepo wa Bwana, na hivyo kujiandaa kukutana naye na kutoa jibu,
Ndiyo, na iwe kama ulivyosema. Ni hofu inayotakiwa kuwa katika kila moyo wa mtu,
kusikiliza iwapo Bwana anagonga, subira yenye kumfanya mtu aboreshe maisha yake ,
kuwa karibu na watu wengine na Mungu.
Na Papa Francisko alihitimisha tafakari
yake , akikumbuka unyenyekevu na ukimya wa Mtakatifu Yosefu na Maria kwamba, ni mwaliko
kwa watu wote, kumkaribisha Yesu kwa uwazi; yeye anayekuja na kuleta zawadi ya amani:
"amani duniani kwa wale ambao neema yake anakaa" ((Luka 2, 14). “Zawadi ya thamani
ya Krismasi ni amani, imani yenyewe ni Kristo. Kristo anayegonga kwenye milango ya
mioyo yetu kwa ajili ya kuijaza mioyo na amani yake. Fungueni milango kwa Kristo.