Papa akutana na wasaidizi wake kutakiana heri za siku kuu ya Noeli
Jumatatu mapema , Papa Francisco, alikutana na wasaidizi wake, wakuu wa Idara na maofisa
wa ngazi ya juu katika Ofisi za Curia ya Roma, katika ukumbi wa Mtakatifu Clementina,
ndani ya Vatican, kwa lengo la kutakiana heri za Krismasi.
Akiwahutubia viongozi
hao , alionyesha kufurahia jadi hii ya kukutana wakati wa mwisho wa kipindi cha
majilio kwa ajili ya kutakiana heri, kwa sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana; tukio la
Mungu aliyefanyika mwanadamu ili kuwaokoa watu, udhihirisho wa Mungu anayekuja kukaa
kwetu, siri ya Mungu ambaye anachukua yeye mwenyewe, hali yetu ya kibinadamu na
dhambi zetu, na kutufunulia maisha yake ya Kimungu, neema yake kubwa na msamaha wake
wa bure. Papa aliendelea kueleza kwamba, ni yeye Yesu , aliyechaguliwa na Mungu,
kuzaliwa katika hali ya umaskini ndani ya pango la Bethlehemu, kutufundisha nguvu
ya unyenyekevu. Na hivyo kwa kweli, Krismasi pia ni sikukuu ya mwanga ambayo si
tu kwa watu walioteuliwa, lakini kwa watu maskini, watu wa kawaida wanaosubiri wokovu
wa Bwana."
Papa ameitumia nafasi hii kutoa shukurani zake za dhati kwa wakuu
hao katika Curia ya Roma, wake kwa waume hasa kwa majitoleo yao ya kuhudumia Jimbo
Takatifu na Kanisa Katoliki la Ulimwengu, na hasa Kiti Kitakatifu na Khalifa wa Mtume
Petro. Papa pia aliwataja hata wale wanaostaafu kwa wakati na pia wale ambao Bwana
amewaita nyumbani kwake , akisema wote wako katika mtima wa moyo wake. Na ameomba
msamaha wa dhati kwa mapungufu yake , kimawazo, kimaneno na kimatendo.
Papa
katika hotuba yake , iliyo angalisha katika Siku kuu ya Noeli, alilenga zaidi hasa
wenye madaraka makubwa na mamlaka, kukumbuka kusitawisha roho wa huduma katika shughuli
zao zote.
Aliasa kwamba, mara nyingi , viongozi hulemewa na kishawishi cha
kujisikia wao ni mabwana wa wanyonge. Ni Mabwana kwa kila mtu na kila jambo, wakisahau
kwamba, ni roho wa upendo, anayetakiwa kuhamasisha maisha yao ya huduma kwa kanisa
la Ulimwengu , ni roho wa unyenyekevu na hasa katika mtazamo kwamba, hakuna mwenye
mastahili au sifa za kuendelea kuishi milele katika dunia hii.
Papa ametaja
majivuno kuwa ni ugonjwa mbaya wenye kuua. Roho huyo wa kujisikia ni bora au muhimu
kuliko wengine ni kati ya maradhi mabaya ya dhambi kumi na tano. Papa alieleza na
kutolea mfano wa roho ya Marta kwa Maria ,katika upangaji na ufanikishaji wa mipango,
akisema, si kuvaa roho wa malalamiko daima, lakini wakati wa kuhudumia, wanapaswa
kutenda siku zote bila malalamiko mengi.
Papa ametaja maradhi haya pamoja
na matatizo mengine na majaribu mengine , huwa ni hatari kwa kila Mkristo na kwa
yoyote aliye pewa dhamana ya kutawala iwe shirika, jumuiya, mabaraza, Parokia,au vyama
vya kikanisa nk, huweza kujenga mgomo katika yote kama mtu binafsi au katika ngazi
ya shirika. Papa aliwakumbusha wakuu hao wa Idara kwamba, ni roho Mtakatifu peke
yake, anayeweza kudumisha kila juhudi ya kweli katika utakaso na kila hamu halisi
kwa ajili ya uongofu. Ni yeye huyo, anayewafanya kuelewa kwamba, kila mfanyakazi ,
anatakiwa kushiriki katika utakaso wa [fumbo] mwili Kristo, ambalo ni kanisa.
"Kwa
hiyo, Papa aliwaambia, wakati huu wa kipindi cha Noel , na kama ilivyo katika muda
wote wa mwaka mzima wameitwa katika kuhudumia, kwa mujibu wa ukweli wa Kazi kwa upendo,
na kukua katika kila njia, katika yeye aliye kichwa, Yesu Kristo, kama mwili mzima
wa Kanisa uliojengeka katika upendo.