Kardinali Jean-Louis Tauran ateuliwa kuwa Camerlengo mkuu
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Kardinali Jean-Louis Tauran, Rais wa Baraza la Kipapa
la Majadiliano ya Kidini, kuwa Camerlengo mkuu wa Kanisa Katoliki. Huyu ni kiongozi
mkuu wa shughuli za Kanisa wakati kunapotokea kwamba, kiti cha Khalifa wa Mtakatifu
Petro kiko wazi kwa sababu mbali mbali. Baba Mtakatifu amemteua Askofu mkuu Giampiero
Gloder, Rais wa Baraza la Taasisi za Kanisa kuwa Msaidizi wa Camerlengo mkuu.
Itakumbukwa
kwamba, kabla ya mabadiliko haya, Camerlengo mkuu wa Kanisa Katoliki alikuwa ni Kardinali
Tarcisio Bertone ambaye alikuwa pia Katibu mkuu wa Vatican wakati wa uongozi wa Baba
Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI.