Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake
hiyo kuanzia Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu. Katika barua yake
kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri
wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali
ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa
na uaminifu na uadilifu.