Baba Mtakatifu Francisco , mapema Alhamisi , Kanisa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
hapa Vatican, aliongoza Ibada ya Misa ya wafu kwa ajili ya kifo cha Kardinali Jorge
Maria Mejia, Mkutubu Mstaafu, aliyefariki mjini Rome, siku ya Jumanne 9Desemba, akiwa
na umri wa miaka 91. Na ibada ya Mazishi iliongozwa na Mkuu wa Dekania ya Makardinali,
Kardinali Angelo Sodano, akishirikiana na umati wa Makadinali wapatao thelathini,
akiwemo Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, pia Maaskofu wakuu wanne na
kundi na Maaskofu. Marehemu Kardinali Jorge Mar’a Mejìa, amezikwa katika kanisa
lake la Mtakatifu Jerome wa Upendo , lililoko katika uwanja wa Farnese, jijini Roma.
.
Kardinali Angelo Sodano, katika homilia yake , alisema , "kwa mpendwa wetu
Kardinali Jorge Mejía, umefika wakati wake wa kurejea katika nyumba ya Baba, baada
ya kuishi katika dunia hii, kwa uwepo mzuri wa umri wa miaka tisini, ambayo aliishi
katika mwanga wa imani, kwanza katika nchi yake pendwa ya Argentina na baadaye hapa
mjini Roma, katika huduma ya Kiti Kitakatifu. Aliteuliwa kuwa mtumishi katika Kiti
Kitakatifu na Papa Paulo VI, mwaka 1977,kama Katibu wa Tume ya Mahusiano na Uyahudi.
Kardinali
Sodano , aliendelea kueleza historia ya Marehemu Kardinali Jorge kwamba, daima alibeba
ndani ya moyo wake kimyakimya urithi wa utamaduni kiteolojia , aliojipatia baada ya
masomo yake huko Buenos Aires na kisha kukamilishwa hapa mjini Roma, katika Chuo
ch Kipapa cha Angelicum na Taasisi ya Kipapa ya Biblia. Ni mtu aliyekuwa ameyatolea
maisha yake kama mtaalam wakati wa mchakato wa Mtaguso Mkuu wa II, katika miaka ya
1963-1964, na baadaye mwaka 1977, aliletwa karibu na Makao Makuu ya Jimbo Takatifu
, kwa ajili ya kutoa mchango wake wa thamani katika ofisi mbalimbali, kwanza kwa
utawala wa Papa Paulo VI na kisha Papa Yohana Paul II, katika Baraza la Haki na Amani,
katika Usharika kwa ajili ya Maaskofu na Maktaba Vatican.
Na hivi karibuni
, alipatwa na maradhi yenye kuwa na maumivu makali, yaliyo rudisha nyuma , utendaji
wake, na alitumia siku zake mwisho kwa utulivu mkubwa, akimwiga Musa, aliyewaambia
wana wa Israel, wakati wakielekea nchi ya ahadi "kumtazama yeye asiyeonekana."
Ilikuwa mtazamo huohuo pia ulio andikwa na Papa Paulo VI katika maandishi yake maarufu
"Juu ya Wazo la kifo." "Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa ndugu yetu mpendwa Jorge,
ambaye alitumia siku zake za mwisho kuombea uenezaji wa Ufalme wa Mungu.
Siku
za hivi karibuni kabla ya kifo chake, Kardinali Sodano alikwenda mjulia hali na kumfariji,
na maneno sisi sote tuko katika mikono ya Bwana , naye mgonjwa alifungua macho yake
na kusema, tupo katika mikono mizuri . Kardinali Sodano , alisema, na hilo ndilo
tumaini la kila Mkristo , kukamilisha safari ya maisha ya hapa duniani , kwa imani
ya kwenda katika mikono ya Bwana. “Hii ni hekima ya Kikristo ambayo ili angazia njia
ndefu ya ndugu yetu mpendwa Jorge. Na maisha yake yamebaki daima kuwa mfano wa kuishi
katikati yetu, na kwa taifa lake pendwa la Argentina”. Tunamwobea pumziko la amani
katika mikono ya Bwana aliyemtumikia.