2014-12-10 16:10:01

Ujumbe wa Papa kwa Mkutano wa Vienna wa Katazo la Silaha za Nyuklia.


Kwa ajili ya Mkutano unaozungumzia madhara ya silaha za nuklia, uliofanyika kwa muda wa siku mbili mjini Vienna, 8-9 Desemba 2014, Baba Mtakatifu Francisko, alipeleka salaam na ujumbe wake kwa washiriki wa Mkutano huo kupitia Rais wa Mkutano Waziri Sebastian Kurtz , ambaye ni Waziri wa Shirikisho la Ulaya , Mahusiano na ushirikiano na mataifa mengine katika Jamhuri ya Austria, ambaye pia ni Rais wa Baraza juu ya kishindo cha madhara ya silaha za nuklia kwa binadamu. Mkutano huu , ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Mataifa mbalimbali na mashirika ya kimataifa, na vyama vya kiraia.

Baba Mtakatifu katika salaam na ujumbe wake , amezitaja silaha za nuklia kuwa tatizo la kimataifa, na lenye kuathiri mataifa yote, athari si kwa binadamu wa leo tu lakini pia kwa vizazi vijavyo na hata sayari ambayo ni makazi ya viumbe. Na hivyo ni lazima mataifa kuzingatia Maadili kama hitaji la lazima kupunguza tishio la nyuklia kwa kusitisha uzalishaji na matumizi ya silaha za nyuklia. Kwa hiyo leo hii kuliko hata siku za nyuma , kiteknolojia, kijamii na kisiasa unakuwa ni wito makini wa kidharura , kujali maadili ya Umoja Kama Papa Yohana Paulo II, alivyohimiza siku za nyuma katika waraka wake ( Sollicitudo Rei Socialis 38), ambao unahamasisha watu kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya dunia salama zaidi, iliyosimikwa katika mizizi ya maadili na uwajibikaji katika ngazi ya kimataifa.

Papa Francisco ameendelea kuyataja madhara ya silaha za nuklia kwa binadamu , yanayo tabiriwa na yenye kuathiri pia dunia, akionyesha kujali kwamba, mara nyingi madhara ya nuklia yakizungumziwa hulenga zaidi katika mauaji mengi. Lakini pia ni muhimu, Papa anashauri , lazima kutazama kwa kina zaidi mateso yasiyokuwa ya lazima hata kwa mtu mmoja mmoja, yanayo sababishwa na matumizi ya silaha hizi za nyuklia. Na kwamba, iwapo mateso hayo yatakomeshwa katika matumizi ya mifumo ya kijeshi na sheria za kimataifa, miongoni mwa mengine, vivyo hivyo silaha hizo hazitatumika hata katiakvita vya kawaida.
Maelezo ya Baba Mtakatifu Francisco, yamerejea waathirika na silaha hizo, akisema kwamba , hutoa onyo kwa dunia, kutorudia makosa ya nyuma, yaliyo sababisha athari hizo zisizo rekebishika hata kwa viumbe wengine.

Na kwa moyo wa kibaba, Papa aliwakumbuka waathirika wote wa silaha za nyuklia akitoa mfano wa eneo Hibakusha, na pia waathirika wengine wote wa silaha za nyuklia, ambao sasa wamekuwa rejea na kipimo muhimu kwa mkutano wa Vienna.

Papa amesema,waathirika hao ni sauti ya kinabii , katika mkutano huo, inayolilia familia ya binadamu kuthamini zaidi ya uzuri wa upendo, ushirikiano na udugu , wakati wakijikumbusha hatari ya silaha za nyuklia duniani , zenye kuwa na uwezo wa kuangamiza binadamu na ustaarabu wote.

Papa Francisco anaamini kwamba, hamu ya amani na udugu, itapandikizwa katika kina kirefu katika moyo wa binadamu, na kutoa matunda thabiti mazuri katika njia zake za kuhakikisha kwamba silaha za nyuklia zimepigwa marufuku mara moja na kwa muda wote, kwa ajili ya manufaa ya viumbe wote. Na kwamba usalama wa maisha ya binadamu hata kwa siku za baadaye unategemea sana uhakika wa usalama na amani ya watu wengine, kwa kuwa, iwapo amani, usalama na utulivu havina uhakika kimataifa, hakuna mwenye kuwa na furaha kamili.

Papa ameasa watu wote iwe kama mtu mmoja mmoja au kimakundimakundi na wote kwa pamoja wana wajibika na usalama wa mazingira iwe kwa sasa na hata kwa vizazi vijavyo. Ni matumaini yake makubwa kwamba wajibu huu, utakuwa ni kigezo katika jitihada za wazo la kusitisha silaha za nyuklia, ili dunia iwe huru na silaha hizo za hatari na ni , jambo linalowezekana.








All the contents on this site are copyrighted ©.