2014-12-09 09:51:17

Papa :Tufundishe Mama jinsi ya kwenda kinyume na mawimbi ya dhambi


(Vatican Radio) Kama ulivyo utamaduni wa kila mwaka kwa Papa ,wakati wa Maadhimisho ya Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili , Papa Francisco alikwenda katika Uwanja maarufu wa Piaza Spagna, kwa heshima ya Mama bikira Maria, Mkingiwa dhambi ya asili. Mahali hapo kuna sanamu ya Mama yetu, iliyowekwa juu ya mnara mrefu, ulio karibu na ngazi maarufu za Spagna , katikati ya jiji la Roma. Sikukuu ya Maria Kukingiwa dhambi ya asili ni moja ya matukio yanayoonyesha ukamilifu waMariamu na hivyo kuwa ishara kubwa ya matumaini kwa Kanisa na kwa dunia.

Kwa mwaka huu, katika maadhimisho haya yanayoheshimiwa sana Italia, na kutambuliwa kama ni siku ya mapumziko hata kiserikali, Papa Francisko , kama pia Askofu wa Jimbo la Roma, aliipamba Siku Kuu hii , kwa kutoa zawadi ya sanamu ya Bikira Maria na Mtoto Yesu , kwa Makao Makuu ya Jimbo la Roma , ambayo yako katika Kanisa Kuu la Yohana wa Laterano. Sanamu hiyo ya Maria na Mtoto Yesu, ina historia ndefu ya tangu karne ya XII. Upelekaji wa sanamu hiyo kutoka Makumbusho ya Vatican hadi Kanisa kuu la Laterano , ulikamilika kwa maandamano makini, mapema Jumatatu , ikifuatiwa na Ibada iliyoongozwa na Makamu wa vika wa jimbo la Roma , Askofu Mkuu Filippo Iannone.

Baba Mtakatifu akiwa katika uwanja wa Spagna, alitoa maombi yake kwa Mama Maria Mkingiwa dhambi ya Asili kama ifuatayo:
“O Maria, Mama yetu, Leo watu wa Mungu wako katika maadhimisho ya kutoa heshima kwako , aliyeumbwa bila dhambi ya asili. Tunaomba upokee zawadi ninayo kutolea kwa niaba ya Kanisa la Roma, na dunia nzima. Kwa utambuzi kwamba wewe , ambaye ni mama yetu, ambaye tangu kuumbwa kwako uliwekwa huru dhidi ya dhambi , hili linatupa faraja kubwa. Na kwa kujua kwamba, kwako mabaya hayana uwezo, tunajazwa na matumaini na ujasiri, wa kumpambana na vikwazo vinavyo tukabili kila siku , kutenda dhidi ya vitisho ya yule mwovu.
Na pia tunajua kwamba hatuko peke yetu katika mapambano haya, wala sisi si watoto yatima, kwa sababu Yesu, kabla ya kifo chake juu ya msalaba, alitupatia wewe kuwa mama yetu .

Hivyo sisi, licha ya kuwa wenye dhambi, sisi ni watoto wako , watoto wa Mama aliyekingiwa dhambi asili, watoto tulioitwa katika utakatifu ambamo kwako wewe uliangaziwa neema ya Mungu tangu mwanzo. Kwa hamasa na tumaini hili, tunaomba leo hii ulinzi wako mama, kwa ajili yetu, kwa familia zetu, kwa ajili ya mji huu, na kwa dunia nzima”.

“Nguvu ya upendo wa Mungu, ulio kuhifadhiwa kutoka dhambi ya asili, kwa maombezi yako ya bure ubinadamu uweze kutoka katika utumwa wa kiroho na kimwili, na kuwa na moyo wa kushinda majaribu, kwa kadri ya mpango wa wokovu wa Mungu. Tunatambua kwamba, hata katika sisi, watoto wako, kwa neema yako tunaweza kukishinda kiburi cha mwovu, na tunaweza kuwa na huruma, kama Baba yetu wa mbinguni alivyo na huruma.

Katika wakati huu ambayo tunaongozwa katika kuadhimisha sikukuu ya Kuzaliwa Yesu, tufundishe kukataa dhambi , kuwa watu wa kukutegemea wewe, kuwa watu wa ibada , wanyenyekevu, na wenye kusikiliza, kuwa wakimya , tukizama katika kutafakari hali ya maisha yetu wenyewe, na kutengeneza nafasi nzuri kwa uzuri wa Mungu, chanzo cha furaha ya kweli. O Mama yetu uliye kingiwa dhambi ya asili, utuombee sisi .

Mwisho wa sala hii Papa alisalimiana na wagonjwa wengi waliokuwa wamefika katika uwanja huu wa Spagna , na pia kwa waamini wote waliokuwa wamejazana katika uwanja huu.








All the contents on this site are copyrighted ©.