Balozi Pereira kutoka Costa Rica awasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francisko
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe Mosi, Desemba 2014 amepokea hati za utambulisho
kutoka kwa Bwana Marco Vinicio Vargas Pereira, Balozi mpya wa Costa Rica mjini Vatican.
Bwana Pereira alizaliwa tarehe 30 Agosti 1954. Baada ya masomo yake alijipatia shahada
ya uzamivu kutoka Chuo kikuu cha Costa Rica na baadaye alijiendeleza katika masomo
ya uhusiano na sheria za kimataifa.
Balozi Pereira amewahi kuwa mfanyakazi
katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje naushirikiano wa kimataifa kuanzia mwaka 1975
- 1978; Katibu mkuu wa Ubalozi wa Costa Rica nchini Brazil kuanzia mwaka 1979 hadi
mwaka 1982. Baadaye kuanzia mwaka 1983 hadi mwaka 1989 aliteuliwa kuwa ni Mkuu wa
Idara; Wizara ya Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kuanzia mwaka 1990
- 2003 alikuwa ni Mkurugenzi mkuu na Mshereheshaji mkuu wa taifa. Kunako mwaka 1992
hadi mwaka 1994 alikuwa ni mfanyakazi katika Ubalozi wa Costa Rica nchini Marekani.
Kati ya Mwaka 1998 hadi mwaka 2000 akateuliwa kuwa Balozi wa Costa Rica huko
Belize. Kunako Mwaka 2003 hadi mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Waziri mdogo wa mambo ya
nchi za nje na kunako Mwaka 2006 hadi mwaka 2014 alikuwa ni Balozi wa Costa Rica nchini
Uruguay.