Vitendo vya kigaidi Nigeria vinaendelea kusababisha maafa makubwa!
Rais Giorgio Napolitano wa Italia, amemwandikia ujumbe Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria
kuonesha masikitiko yake kutokana na mauaji ya kinyama yaliyotokea Ijumaa huko Kano,
Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha watu zaidi ya 100 kupoteza maisha na wengine
135 kujeruhiwa vibaya, wakati walipokuwa wanasali kwenye Msikiti mkuu wa Kano.
Mauaji
ya kinyama kutokana na misimamo mikali ya kidini ni jambo ambalo haliwezi kukubalika
kuna haja kwa wananchi wa Nigeria kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa kujifunga
kibwebwe kupambana na vitendo hivi vya kigaidi. Rais Napolitano anapenda kutoa salam
zake za rambi rambi kwa wote walioguswa na maafa haya na kwamba, wasikate tamaa kujenga
na kuimarisha umoja wa kitaifa kama njia ya kupambana na vitendo vya kigaidi.
Vitendo
vya kigaidi nchini Nigeria katika kipindi cha miaka sita nchini NIgeria vimepelekea
uharibifu mkubwa wa nyumba za Ibada, shule, vituo vya Polisi, kambi za kijeshi na
majengo ya Serikali. Rais Jonathan anasema wahusika watasakwa ili kufikishwa kwenye
mkondo wa sheria!