Vyombo vya habari kamwe visiwe visima vya uchochezi na ghasia.
Baba Mtakatifu Francisco Alhamis alikutana na familia ya Mtakatifu Paulo ambao ni
mashuhuri katika uwanja wa habari na mawasiliano. Wawakilishi wa Familia hii ya Mtakatifu
Paulo ambao kwa kifupi hujulikana kama Wapaolini, walimtembelea Papa Francisco kama
sehemu ya hija yao katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. kwa ajili ya kutimia miaka
mia ya kuanzishwa kwa shirika lao na Mwenye Heri Giacomo Alberione. Papa katika
hotuba yake kwa Wapaolini, aliwaambia Wakristo wote kwamba, wana jukumu la kutangaza
Injili , bila ya kubagua mtu. Na kwamba ,maadhimisho ya miaka mia, aliongeza Papa
ni fursa nyingine mpya, ya kufanya upya imani katika maisha na mawasiliano, hasa kwa
njia ya zana uchapishaji na vyombo mbalimbali vya mawasiliano.
Watu watu wote
na wajishughulishe na kutangaza habari njema ya kwamba Mungu ni upendo. Na kwa maneno
ya Yesu, "Uhuru mmepokea bure , toeni bure", Papa aliitaja aya hii kuwa ni siri
ya uinjilishaji. Kwamba, kuiwasilisha Injili , katika mtindo wake wa kiinjili, ni
neema ya bure, bila kuitokea jasho. Ni kiinua mgongo kwa Mkristo, hasa muumini anaye
pokea kwa furaha na upendo safi na kuiwasilisha zawadi hii ya upendo kwa wengine,
kupitia huduma, Ukarimu na upendo.
Hata hivyo, Papa aliongoza, ni tu kwa kufanya
kazi kwa furaha, kunakoweza kutengeneza mawasiliano ya kweli miongoni mwa watu. Ni
vigumu kuwasilisha neno la furaha iwapo anayewasilisha halifurahii neno hilo. Na
ndiyo maana wale walio pokea ujumbe wa Injili kwa furaha wanaweza kuiwasilisha furaha
hiyo kwa wengine. Mawasiliano mazuri ni mzizi wa mafanikio ya kukua kiroho, Papa
alieleza na kurejea Waraka wake wa Kichungaji wa Injili ya Furaha (Evangelii gaudium,
9).
Kuinjilisha, kimsingi, ni kutangaza Injili "kwa wale ambao hawajui Yesu
Kristo au kwa wale wanaoikataa. Kwa msukumo huo, Papa Francisco alisisitiza kuwa ,
inakuwa ni haki ya kila Mkristo kuitangaza Injili bila kumbagua mtu .Na kwao Wapaolini
, kama Wakatoliki, DNA ya damu yao, inapaswa kuwa ukatoliki, kama ilivyokuwa kwa
mwanzilishi wa shirika lao, wakivuviwa na maisha na utume wa Mtakatifu Paulo. Papa
aliendelea kulitaja Kanisa kuwa ni mfano wa Msafiri, mwenye kuonyesha tumaini lake
kwa Kristo. Wakristo ni Kanisa hujaji, ambalo mizizi wake ni kumtangaza Kristo
na upendo wake kwa viumbe wote, kufungua vifundo vyote vya pingu za mitindo ya maisha
ya kidunia, na kuweka wazi roho na uwezo wa mitazamo na matukio kwa neema ya Bwana.
Ujumbe wa Papa unasema, bado kuna wengi wanasubiri kumjua Yesu Kristo. Ndoto
ya upendo usiojua mipaka isipokuwa kufungua barabara mpya kuleta pumzi mpya ya Injili
katika tamaduni na katika maeneo mbalimbali ya jamii.Huu ni wito wa kitume kwa ajili
ya wogofu wa mtu binafsi na jamii . Na ni tu mioyo iliyo wazi katika kuipokea neema
hii ya mahusiano inayoweza kupata uelewa na maana ya ishara za nyakati na kutoa wito
katika hitaji la kibinadamu, matumaini na amani.
Alikamilisha kwa kuwalenga
Wapaolini akisema , katika njia yao ya kumfuata Kristo na kwa ushuhuda wao, ni wazi
Mwaka kwa ajili ya Maisha yaliyowekwa Wakfu utaweza kuwa msaada Mkubwa katika maisha
yao ya kitawa na katika kulitumikia kanisa na dunia kwa ujumla.Papa alieleza na kuwatakia
baraka za Bwana katika shughuli zao za kila siku.