2014-11-28 12:35:24

Matumaini ya Italia kwa hija ya Baba Mtakatifu nchini Uturuki


Rais Giorgio Napolitano wa Italia anamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa ujumbe na matashi mema kwa ajili ya Italia na wananchi wake. Anamtakia kheri na baraka tele katika hija yake ya kiekumene huko Uturuki, nchi ambayo kwa sasa ina mchango mkubwa katika kutafuta suluhisho la amani kwa maelfu ya watu wanaoteseka kutokana na vita inayoendelea huko Mashariki ya Kati, ambayo imepelekea watu wasiokuwa na hatia kupoteza maisha yao!

Ni matumaini ya Rais Napolitano kwamba, hija hii ya kiekumene itasaidia kukoleza ari na moyo wa majadiliano kati ya Mashariki na Magharibi; kati ya Waamini wa dini ya Kiislam na Kikristo; ili kujenga na kudumisha matumaini kwa kesho iliyo bora zaidi, kwa kutambua tofauti kati ya watu na dini zao, kama utajiri na wala si kikwazo kati ya watu.







All the contents on this site are copyrighted ©.