2014-11-24 11:34:02

Papa akutana na mahujaji kutoka India


(Vatican Radio) Mapema Jumatatu, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kundi la mahujaji kutoka India, waliofika Roma kwa ajili ya kutajwa Mtakatifu mwenzao Mtumishi wa Mungu Padre Kuriakose Elias Chavara na Sista Euphrasia Eluvathingal.

Baba Mtakatifu katika hotuba yake fupi kwa mahujaji hao, alitafakari juu ya maisha ya Mtakatifu Mpya , Padre Kuriakose Elias, akisema, akilitumikia kanisa kama Mtawa, aliyatolea maisha yake kupitia kazi zake kwa uaminifu, ukarimu na unyenyekevu wa hali ya juu, kwa ajili ya kanisa la Syro-Malabar, na katika utakaso wake binafsi na kwa ajili ya wokovu wa wengine. Pia Papa alimzungumzia Mtakatifu Sista Euphrasia, kwamba aliishi katika muungano kushangaza na Mungu hivyo kiasi kwamba maisha yake ya utakatifu, yanakuwa mfano hai na kutia moyo kwa watu, hadi watu wakamwita “Mama wa maombi ."

Papa Francisco , kwa namna ya kipekee, alitoa shukurani zake kwa juhudi zinazofanywa na Kanisa katika Jimbo la Kerala, hasa kwa bidii yao ya kitume, na kwa kuwa shahidi wa imani, na shamba lenye rutuba nzuri katika miito ya kidini na ukuhani.
Papa aliendelea kutoa shukurani zake za dhati pia kwa viongozi wa kanisa, kwa Kardinali George Alencherry, kwa Maaskofu na mapadri, wanaume na wanawake Watawa , walei na kwa kila muumini wa Kanisa la Kanuni ya Syro-Malabar. Na pia kwa ajili ya wingi wao kufika Roma kushiriki katika tukio hili muhimu sana, na kuwa na uwezo wa kuishi siku ya imani na ushirika wa kikanisa, pia kutolea sala na maombi katika makaburi ya Mitume. Papa aliwaomba wakati huu wa Ibada na tafakari kali za kiroho, uweze kuwasaidia kutafakari kazi ya ajabu, iliyokamilishwa na Bwana katika maisha na matendo ya watakatifu hawa wapya.

Uwepo wa maisha yao, na usaidie kuwa hazina katika mafundisho ya maisha ya kiinjili. Kufuata nyayo zao na kuwaiga, kwa namna ya pekee, kwa njia ya upendo wa Yesu katika Ekaristi na upendo wa Kanisa. Hivyo ili pia wao waweze kutembea pamoja nao katika njia ya utakatifu. Kwa tumaini hili na uhakika wa sala zake, Papa aliwatakia kila mmoja wao, na watoto wao wapendwa, Baraka zake za Kitume. Asante!








All the contents on this site are copyrighted ©.