2014-11-23 09:12:34

Watu 28 wauwawa kikatili nchini Kenya kwa vile hawakujua kusoma Koran Tukufu!


Serikali ya Kenya imewahakikishia wananchi wake kwamba, itawasaka kwa udi na uvumba wale wote waliohusika na mauaji ya kinyama ya watu 28 ambao sio wa dini ya Kiislam kwa vile walishindwa kusoma Koran, ili kuwafikisha kwenye mkondo wa sheria.

Ni maneno mazito yaliyotolewa na Bwana Willim Ruto, Makamu wa Rais wa Kenya, wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kenya kwa njia ya Televisheni baada ya Magaidi wanne wa Kikundi cha Al Shabaab kuteka nyara Bus na hatimaye kufanya mauaji ya kinyama.

Kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab, Jumamosi, tarehe 22 Novemba 2014 kimejigamba kwa kusema kwamba, wanamgambo wake wameteka Bus lililokuwa linasafiri karibu na mpaka wa Kenya, Somalia na Ethiopia na kuwauwa "Kafiri" 28, kama kitendo cha kulipiza kisasi kutokana na upekuzi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwenye misikiti kadhaa inayoshukuwa kutumiwa na vikundi vya kigaidi kuchafua amani na utulivu nchini Kenya.







All the contents on this site are copyrighted ©.