2014-11-18 14:08:04

Rais Macky Sall wa Senegal akutana na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne, tarehe 18 Novemba 2014 amekutana na kuzungumza na Rais Macky Sall wa Senegal ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, aliyekuwa Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili wameridhika na mahusiano mazuri yaliyoko kati ya pande hizi mbili pamoja na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa katika sekta ya elimu, afya na katika mchakato wa majadiliano yanayopania pamoja na mambo mengine kujenga na kudumisha umoja wa kitaifa. Baba Mtakatifu na mgeni wake, wamegusia pia masuala ya kimataifa na kwa namna ya pekee, kinzani za kisiasa zinazoendelea kujitokeza Afrika Magharibi.







All the contents on this site are copyrighted ©.