2014-11-17 11:56:11

Msiyakoroge, kuyakaanga au kuyachemsha!


Jumuiya ya wanafunzi Wakatoliki pamoja na Watanzania wanaoishi na kufanya kazi mjini Roma, Jumapili tarehe 16 Novemba 2014, walikutana kusali kwa ajili ya kuomba baraka na neema kwa Mwaka wa masomo 2014- 2015; kuombea amani na ustawi nchini Tanzania; Kumkumbuka Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, pamoja na kumwombea afya njema Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania aliyefanyia operesheni hivi karibuni huko Marekani. RealAudioMP3

Ibada ya Misa Takatifu ilifanyika kwenye Seminari kuu ya Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu, Kanda ya Italia na kuhudhuria na umati mkubwa wa Mapadre, Watawa, Waseminari na Waamini walei. Balozi James Msekela na Familia yake walihudhuria pia. Ibada ya Misa Takatifu imeongozwa na Mheshimiwa Padre Alcuin Nyirenda, OSB aliyekazia umuhimu kwa waamini ambao ni wajasiria mali kuchakarika ili kuhakikisha kwamba, wanatumia hekima katika kupima na kutenda, ili wasije wakayakoroga, kuyakaanga au kuchemsha!







All the contents on this site are copyrighted ©.