Baba Mtakatifu Francisko, hivi karibuni alipata fursa ya kusikiliza nyimbo mbali mbali
zilizoimbwa wakati wa mkutano wa Makardinali walipokuwa wanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi
hadi siku ile Baba Mtakatifu Francisko alipoanza utume wake rasmi, kama Khalifa wa
Mtakatifu Petro.
Hizi ni nyimbo zilizokusanywa katika CD mbili na zimeimbwa
na Kwaya ya Kikanisa cha Sistine. Kwa sasa CD hizi inauzwa kwenye maduka mbali mbali
nchini Italia na baada ya muda si mrefu CD hizi zitaweza kupatikana kwa watu wengi
zaidi. CD hizi zimetengenezwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya Deutsche Grammophon
kutoka Ujerumani kwa kushirikiana na Radio Vatican.
Uzinduzi wa CD hizi ulihudhuriwa
na viongozi kadhaa kutoka Vatican akiwemo Monsinyo Massimo Palombella, Mkurugenzi
wa Kwaya ya Sistine, Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican na Mkurugenzi
wa Radio Vatican pamoja na viongozi na wafanyakazi kutoka Kampuni ya Deutsche Grammophon
ya Ujerumani. CD hii inakwenda kwa jina la "Habemus Papam" yaani "Tumepata Papa".