2014-11-13 14:26:19

Rais wa Austria akutana na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 13 Novemba 2014 amekutana na kuzungumza na Bwana Heinz Fischer, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Austria ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa amefuatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, aliyekuwa Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Viongozi hawa katika mazungumzo yao, wameonesha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya pande hizi mbili pamoja na kujadili masuala ya kimataifa, hususan umuhimu wa kudumisha uhuru wa kidini na haki msingi za binadamu; sanjari na watu kujikita katika mchakato wa majadiliano ya kidini na kitamaduni. Mwishoni, viongozi hawa wawili wamejadiliana kuhusu masuala tete ya kimataifa na hasa zaidi hali ilivyo huko Mashariki ya Kati.







All the contents on this site are copyrighted ©.