Ufalme wa Mungu hukua kila siku ndani mwa Wale wanao ushuhudia kimyakimya bila kelele,
wakisali na kuuishi imani yao mahali pote, ndani ya familia, kazini,mashambani na
katika mikutano na kukutana wengine, alieleza Papa Francisko, mapema asubuhi Alhamisi,
wakati akiongoza Ibada ya Misa katika katika Kanisa dogo Mtakatifu Marta, Vatican.
Katika homilia yake, Papa aliutaja ukimya huo kwamba ni muhimu hata pale kunapokuwa
na kupungukiwa au kuishiwa mahitaji muhimu ya mwili, akisema, inaweza kuwa kimebaki
kibaba kimoja hadi mwisho wa mwezi, lakini iwapo daima kuna maombi, huduma kwa watoto
na wazee, ndani ya nyumba hiyo mna ufalme wa Mungu.Papa anasema, mMbali na kelele
za watu, ufalme wa Mungu huwa na njia zake katika kukua, kama inavyokua mbegu iliyofukiwa
chini ya aridhi bila ya kuwa na kelele huchipuka na kukua kwa kuvutia.
Homilia
ya Papa Francisco, ililenga zaidi katika somo la Injili ya Siku kutoka Mt. Luka,
ambapo Yesu anawajibu waliotaka kujua lini Ufalme wa Mungu atakuja. Yesu anajibu,
siku itakuja watakapo waambia "huyu hapa au yuko kule ,msiende na wala msiwafuate
wao.
Papa Francis alisema Ufalme wa Mungu si tamasha. Kwa wengi hufananisha
ufalme wa Mungu kwamba itakuwa ni tamasha kubwa. Papa alibainisha kwamba, pamoja na
ujio wa Ufalme wa Mungu kuwa ni sherehe kubwa, sherehe hiyo ni tofauti. Kwa hakika
ni sherehe nzuri. Sherehe kubwa. Na Mbinguni itakuwa sherehe, lakini si tamasha. Bahati
mbaya , udhaifu wa binadamu hupendelea zaidi matamasha
Papa aliendelea na mafundisho
yake kwamba, kwa mara nyingi ya Ibada hugeuzwa kuwa kama matasha ya harusi ambako
watu wanapenda kuvaa vizuri mitindo mipya kwa dhamira za kujionyesha wakati wa kupokea
Ekaristi. Huo ni ubatili, kwa kuwa Ufalme wa Mungu umo katika kimya cha ndani ambamo
hupata kukomaa kimyakimya , bila kujionyesha. Roho Mtakatifu huulisha moyo kupitia
nia zake, katika udogo ulioandaliwa vyema kiroho. Na kwa kunukuu maneno ya Yesu Papa
alisema, siku itakuja ambapo Ufalme utakuwa wazi kwa nguvu zake zote, na huo utakuwa
ukamilifu wa nyakati. Siku ambayo yeye atapiga mbiu ,na kutoa mwanga kama radi
, mwanga utakao mulika kama taa ya umeme juu angani kutoka upande mmoja hadi mwingine.
Hivyo ndivyo Mwana wa Mtu katika siku hiyo atakavyo piga kelele. Papa alieleza kwa
kuyaelekeza mawazo kwa familia nyingi zenye kudumu katika uvumilivu , zile zinazohangaikia
kuidumisha familia , wake kwa waume , wanaohudumia watoto, wajukuu hufika mwisho wa
mwezi bila hata ndululu ya fedha iliyobaki katika mfuko wao lakini watu hawa hawakupunguza
sala na maombi yao kwa Kristo, Mwana wa Ufalme wa Mungu. Katika familia hizo , kuna
Ufalme wa Mungu uliofichika katika siri ya maisha ya kila siku , kila siku ni siku
ya takatifu, kwa sababu Ufalme wa Mungu si mbali nao.
Papa Francis iliendelea
kueleza kwamba,, hata katika mateso, na msalaba wa maisha ya kila siku - msalaba
wa kazi, familia, na mambo mengine ya kijamii ni kutenda mema kimyakimya bila kujionyesha,
kwa kuwa msalaba ni sehemu ya Ufalme wa Mungu.
Papa Francisco, alihitimisha
na wito kwa wote,ambamo ameomba kuzidisha sala na maombi,kumwomba Bwana, neema ya
kukua ndani ya Ufalme wa Mungu, ndani mwetu, kwa ibada, huduma ya upendo, ukimya.
Ufalme
wa Mungu ni mnyenyekevu, kama mbegu ilivyokuwa na wa kukaa aridhi na baadaye kukua
ndivyo ulivyo unyenyekevu wa roho ,uliosimikwa kwenye nguvu ya Roho Mtakatifu . Na
hivyo,Papa akasema, ni juu ya kila mtu kuruhusu kukua katika neema ya ufalme wa Mungu
bila majingambo ya kujionyesha kwa mbwembwe, lakini ni kuwa na mabadiliko ya kiroho
yanayo tanguliza mbele ukimya, amani, utulivu, katika kuwa karibu wa Mwenyezi Mungu,
na wengine, katika ibada kwa Mungu, bila tamasha .