Baba Mtakatifu amemteua kuwa msimamizi wa kitume wa Mamlaka ya kijeshi ya Malta, Kardinali
Raymond Leo Burke, aliyekuwa Msimamizi wa Mahakama Kuu Kitume ya Signatura. Na
katika nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Kardinali Burke, imejazwa na Askofu Mkuu Dominique
Mamberti, Askofu Mkuu wa jina wa Sagona, ambaye alikuwa Katibu wa Mahusiano na nchi
zingine kwa Vatican. Katika nafasi yake, Papa amemteua kuwa Katibu kwa Mahusiano
na nchi zingine, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Askofu Mkuu wa jina wa Askofu
Mkuu wa Hodelm, ambaye ni Mjumbe wa Kitume wa Papa nchini Australia.