2014-11-05 08:08:25

Hongera Rev. Dr. Fr. Federico Lombardi, SJ.


Katika maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25 ya Kitivo cha Mawasiliano ya Jamii, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesiani, kilicho mjini Roma, kilichoanzishwa kunako mwaka 1989, kutafanyika kongamano juu ya mawasiliano ya kijamii kwa kuangalia nadharia, teknolojia na mbinu za ufundishaji. Kongamano hili litafanyika kuanzia tarehe 14- 15 Novemba 2014 mjini Roma.

Katika kilele cha maadhimisho haya, Padre Federico Lombardi, Mkurugenzi mkuu wa Radio Vatican na Msemaji mkuu wa Vatican, atatunukiwa Shahada ya juu ya Udaktari wa heshima katika mawasiliano ya jamii kwa kutambua mchango wake katika uwanja huu, utume ambao ameufanya kwa juhudi, bidii, maarifa na majitoleo makubwa, kiasi hata cha kuwashangaza wengi, katika unyofu na unyenyekevu wake anapokuwa katika tasnia ya habari.

Kongamano hili linatarajiwa kutoa dira na mwelekeo katika ufundishaji wa mawasiliano ya jamii kwa siku za usoni kutokana na ukweli kwamba, teknolojia ya mawasiliano inayoendelea kubadilika kwa haraka sana, changamoto ya kujiweka sawa, ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya mawasiliano ya jamii.







All the contents on this site are copyrighted ©.