Siku ya Watakatifu wote, hutukumbusha kifo si mwisho wa maisha yetu
Katika maadhimisho ya Siku Kuu ya Watakatifu wote, Novemba Mosi, Baba Mtakatifu
nyakati za adhuhuri, amehutubia umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekusanyika katika
uwanja wa Kanisa Ku la Mtakatifu Petro, Vatican, pia wakiwepo washiriki wa mbio za
Watakatifu wote.
Katika hotuba yake amekumbusha kwamba, siku hizi mbili za
kwanza za Mwezi Novemba, kwetu sote kama waamini , ni wakati wa kutoa maombi na
tafakari juu ya mwisho ya maisha ya hapa duniani. Na ukweli wake, maadhimisho ya
siku hizi mbili hukumbusha yote mawili , Watakatifu na Waamini Marehemu, wakionyesha
maisha ya kanisa kuwa katika hija kama ilivyo elezwa katika Liturujia ya siku, kuwa
ni dhamana ya kiroho inayo unganisha Kanisa na mbingu. Siku ya Watakatifu wote, ni
siku ya kumtukuza Mungu kwa ajili ya wanaume na wanawake Watakatifu wa umri wote,
na kariba zote ambao waliofikia mwisho wa maisha ya dunia, lakini walianza maisha
mapya kwa Mungu. Wakati huo huo tunawakumbuka wapendwa wetu Marehemu, kwa kutembelea
makaburi, chanzo cha faraja kubwa, katika kufikiri kwamba, wao wameungana na Bikira
Maria, mitume, mashahidi na watu wote wa Mbinguni!
Papa aliendelea kusema,
Maadhimisho ya Sikukuu hii ya Watakatifu wote, hivyo husaidia sisi kufikiria ukweli
msingi wa imani ya Kikristo tunayokiri katika sala ya Nasadiki, Nasadiki katika ushirika
wa watakatifu. Ni ushirika unatokana na imani inayo waunganisha walio wa Kristo kwa
njia ya ubatizo wao. Ni muungano wa kiroho, usioweza kuvunjwa na kifo, lakini unaendelea
katika maisha yajayo. Kwa kweli kuna dhamana isiyovunjika kati yetu, tulio bado katika
dunia hii na wale ambao walivuka kizingiti cha kifo. Sisi hapa duniani, pamoja na
wale ambao wameingia katika milele, huunda familia moja kubwa ya Mungu.
Ushirika
huu mzuri kati ya mbinguni na duniani, unaodhihirishwa kwa kina zaidi katika maadhimisho
hali ya juu na kina, katika Liturujia, na hasa katika maadhimisho ya Ekaristi, inayoeleza
na kuonyesha muungano kamili kati ya wafuasi wa Kanisa. Katika Ekaristi, waamini wanakutana
na Yesu aliye hai na nguvu zake, na kwa njia yake huingia katika ushirika na udugu
katika imani, wale ambao wanaishi nao hapa duniani na wale ambao wametangulia mbele
katika maisha ya pili, maisha kutokuwa na mwisho. Ukweli huu wa ushirika hutuvika
furaha, uzuri na udugu na wote wake kwa waume katika imani ambao hutembea pamoja
kama waamini, wakisaidiana kutembea pamoja katika safari hii ya barabara inayoelekea
mbinguni. Na ni faraja kujua kwamba, kuna ndugu wengine ambao tayari wametangulia
uwinguni, wanaoomba kwa ajili yetu, ili kwamba kwa pamoja tunaweza kutafakari umilele
wa utukufu na huruma ya Baba. Papa Francisko aliendelea kusema, katika kusanyiko
kubwa la Watakatifu, Mungu alipenda kutoa nafasi ya kwanza kwa Mama wa Yesu. Bikira
Maria yuko katikati ya ushirika wa Watakatifu, kama mlezi wa kipekee wa Kanisa zima
la Kristo. Kwa wale wanaopenda kumfuata Yesu kwa njia ya Injili, Bikira Maria huwaongoza
kwa usalama, kwa kuwa yeye ni Mama aliye makini na mwenye kujali, ambaye tunaweza
kumwekea kila nia yetu na matatizo yetu. Papa alieleza na kukamilisha kwa kuwaalika
wote kumwomba Malkia wa Watakatifu wote, atusaide kutoa jibu kwa ukarimu na uaminifu
kwa Mungu, anayetuita kuwa watakatifu kama yeye alivyo Mtakatifu (tazama Law 19.2;
Mt 5:48). Baada ya sala ya Malaika wa Bwana , Papa Francisco pia alitoa mwaliko
kwa wote kuombea Mji Mtakatifu wa Yerusalem, na kwa ajili ya Waamini wa dini kuu
tatu , Waislamu Wayahudi na Wakristo, ambao katika siku hizi wamekuwa ni mashahidi
wa hali za mivutano na wasiwasi, ili waweze kuashiria amani, Mungu anayopenda kuiona
katika familia zote. Pia alirejea tukio la kutangazwa kuwa Mwenye Heri Padre Pedro
kama shahidi wa imani , huko Hispania. Na pia aliwataja na kuwatakia mema, wale wote
walioshiriki katika mbio za Watakatifu wote, ambazo huandaliwa na Chama cha Don Bosco
hapa Roma.