2014-10-28 10:00:06

Ujumbe wa Kikristo unajikita katika furaha, upendo na huruma!


Injili ni moyo wa Maandiko yote Matakatifu kwa vile ni ushahidi mkubwa juu ya maisha na mafundisho ya Neno wa Mungu aliyefanyika Mwili na kukaa kati ya watu wake kwa njia ya Roho Mtakatifu, ili aweze kuwakomboa wanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti. Injili ni uthibitisho wa ukweli wa kihistoria kuhusu maisha na mafundisho ya Yesu hadi siku ile alipopaa mbinguni kwenda kwa Baba yake wa mbinguni.

Nguvu ya Neno na uwezo wa Neno la Mungu ni kubwa hivi kwamba zinaunda kwa ajili ya Kanisa mahali pake pa kutegemea na utendaji wake. Na kwa ajili ya watoto wake, ni nguvu ya imani yao, chakula cha roho zao, chemchemi safi na ya daima ya maisha ya kiroho. Kwa hiyo ni lazima waamini waweze kuyapata kwa wingi na urahisi Maandiko Matakatifu.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawaalika waamini kuwasaidia Watu wa Mataifa kugundua furaha ya ujumbe wa Kikristo; ujumbe unaojikita katika upendo na huruma.











All the contents on this site are copyrighted ©.