2014-10-27 08:55:17

Upendo wa Mungu na jirani hautengani-Papa


Baba Mtakatifu Francisco, Jumapili akiwahutubia mahujaji na watalii waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, alisema, upendo wa Mungu umegubikwa ndani ya upendo kwa jirani. Katika hotuba yake Baba Mtakatifu, alitoa tafakari fupi juu ya somo la Injili ya siku, ambayo ilikuwa kutoka Injili Mtakatifu Mathayo 22: 34-40.

Papa alisema, “Injili ya leo inatukumbusha kwamba sheria zote za Mungu hutuongoza kumpenda Mungu na jirani," na kwamba "Huwezi kumpenda Mungu bila kumpenda jirani yetu na huwezi kumpenda jirani bila kumpenda Mungu. Papa aliendelea kusema kwamba, mafundisho mapya ya Kristo yamo ​​katika muungano wa amri hizi mbili. Aidha aliangalisha katika tafakari ya mtangulizi wake, Papa Mstaafu Benedict XVI, katika barua yake ya kwanza ya Kitume, Mungu ni Upendo ” Deus Caritas est,” kipengere namba 16-18 .

Papa Francisco aliendelea kusema, "Yesu anakamilisha sheria ya agano, kwa umwilisho wake ambamo inamwunganisha yeye mwenyewe, katika mwili wake, umungu wake na ubinadamu wake , katika siri moja ya upendo. Na katika mwanga wa neno la Yesu, upendo unakuwa kipimo cha imani, na imani ni roho ya upendo, na hivyo hatuwezi kutenganisha maisha ya kidini - maisha ya ucha Mungu , na huduma kwa wake kwa waume, kwa ndugu zetu, wenye mwili na damu kama sisi tunaokutana nao.

Baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa Francisco alilikumbuka tukio la kutajwa kuwa Mwenye Heri, Mama Asunta Marchetti, katika Ibada iliyofanyika Jumamosi 25 Oktoba, huko Sao Paulo, Brazil . Mama Assunta Marchetti: mzaliwa wa Italia, ni mwanzilishi wa Shirika la Masista Wamisionari wa Mtakatifu Charles Borromeo, wanaojulikana kama” The Scalabrinians. Alianzisha shirika hilo mwishoni mwa karne ya 19 baada ya Askofu wa Piacenza, Giuseppe Scalabrini, ambaye alisaidia kuanzishwa kwa shirika katika lengo la kudumisha mafundisho ya imani Katoliki na maisha Katoliki miongoni mwa wahamiaji waliokuwa wakiingia katika nchi zilizojulikana kwa wakati ule Dunia Mpya. Mpaka sasa utume wa shirika hilo hulenga zaidi kwa wahamiaji, wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao.

Papa Francisco aliendelea kumtaja Mama Assunta Marchetti kwamba aliiona sura ya Yesu katika watu maskini, yatima, katika wagonjwa, katika wahamiaji. Na hivyo ni jambo la kumshukuru Bwana kwa uwepo wa Mama huyo, ambaye anaendelea kuwa mfano wa roho ya Kimisionari na roho ya kujituma kwa ujasiri bila kuchoka katika huduma ya upendo. Mtumishi huyu wa Mungu anakuwa uthibitisho wa ukweli kwamba, tunaweza na lazima kuutafuta uso wa Mungu kwa watu wote wake kwa waume.

Papa Francis pia alitoa salaam zake kwa mahujaji kutoka pande zote za dunia, na kukitaja rasmi kikundi cha Schoenstatt, ambao siku ya Jumamosi kilikuwa na mkutano wake hapa Roma, na pia aliikumbuka jamii Peru ambayo ilifika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kusali sala ya Malaika wa Bwana, kwa kufanya maandamano wakiwa wamebeba Sanamu ya Kristo Msulubiwa ya “ El Senor de los Milagros” - Bwana wa Miujiza – ambayo ilitengenezwa na mtu aliyewekwa huru karne ya 17 huko Lima. Sanamu hiyo sasa inaheshimiwa sana na watu wa Peru kama kielelezo cha upendo wa kina wa mtu k uyatoa maisha yake kwa ajili ya mwingine na hasa miongoni mwa watu wa Peru.








All the contents on this site are copyrighted ©.