Kura ya maoni kuhusiana na Muswada wa Katiba ni hapo tarehe 20 Aprili 2015
Serikali ya Tanzania umetangaza kwamba, tarehe 30 Aprili 2015, watanzania watapiga
kura ya maoni kuhusiana na Muswada wa Katiba Mpya, kadiri ya tamko lililotolewa na
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Frederick Werema. Muswada wa sheria ambao umepitishwa
hivi karibuni na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao maalum cha
Bunge la Katiba, ndio utakaofanyiwa kazi siku hiyo.
Ikiwa kama Muswada wa Katiba
Mpya utapitishwa, watanzania wanaweza kufanya uchaguzi mkuu kwa kutumia Katiba ambayo
imekumbana na upinzani mkubwa kutoka ndani na nje ya Bunge maalum la Katiba, kiasi
kwamba, baadhi ya wajumbe wakasusia kushiriki vikao vya Bunge.