Baraza la Kipapa la haki na amani kwa kushirikiana na Taasisi ya Kipapa ya Sayansi
Jamii, kuanzia tarehe 27 hadi tarehe 29 Oktoba 2014 kwa pamoja wameandaa mkutano wa
kimataifa kuhusu vyama vya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani utakaofanyika mjini
Roma.
Hivi ni vyama vinavyowawakilisha watu ambao wanaendelea kusukumizwa
pembezoni mwa Jamii kutokana na utandawazi usiojali wala kuthamini utu na heshima
ya heshima ya binadamu. Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa watu
wasiokuwa na fursa za ajira, wahamiaji na wale wanaojihusisha katika mchakato wa kuwajengea
watu uwezo ili kukabiliana vyema na changamoto za maisha.
Kuna wawakilishi
wa wakulima ambao wameng'olewa kutoka katika ardhi yao ili kuwapisha wenye nguvu kuwekeza
katika sekta ya kilimo, makundi ya watu wanaoishi pembezoni mwa miji katika makazi
yasiyokuwa rasmi kutokana na ukosefu wa makazi bora mijini. Baada ya mkutano huu,
wajumbe wanatarajiwa kuanzisha mtandao wa kimataifa utakaosaidia kuratibu shughuli
hizi kwa kusaidiana na Kanisa.