2014-10-19 15:00:18

Mwenyeheri Papa Paulo VI alikuwa ni Nabii shupavu!


Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika mahojiano maalum na Radio Vatican anasema kwamba, Mwenyeheri Papa Paulo VI alikuwa ni Nabii shupavu aliyekuwa na mwono mpana katika kulinda, kutetea na kuendeleza utu, heshima na zawadi ya uhai wa binadamu kadiri ya mpango wa Mungu. RealAudioMP3

Mwenyeheri Paulo VI katika maisha na utume wake, alikazia umuhimu wa binadamu kuzingatia mpango wa Mungu katika kazi ya uumbaji kwa kujikita katika mpango wa uzazi kwa njia ya asili ili kupunguza "majanga" mbali mbali yanayoweza kusababishwa na tabia ya kukumbatia utamaduni wa kifo kwa kuenzi sera za utoaji mimba. Alitetea maisha ya ndoa na familia, akawataka wanandoa kudumisha upendo wa dhati kwa kuenzi uhai.

Hili ni jukumu la waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuhakikisha kwamba, wanasimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha zawadi ya uhai tangu pale mtoto anapotungwa mimba hadi mauti ya kawaida yanapomfika kadiri ya mpango wa Mungu. Ni wajibu wa watu wenye mapenzi mema kukataa katu katu misaada inayodhalilisha utu na heshima ya binadamu; misaada inayokwenda kinyume cha kanuni maadili.







All the contents on this site are copyrighted ©.