2014-10-17 08:10:02

Sala za Masifu ni faraja ya moyo--- Papa


Watu wengi, ni wepesi kutoa sala za kuomba neema, kuliko ilivyo sala za sifa na shukurani kwa Mungu, ingawa sala za kusifu, huleta faraja nyingi moyoni. Papa Francisco alieleza Alhamisi wakati wa ibada ya Misa ya asubuhi, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la Vatican.

Homilia ya Papa, ililenga katika somo kutoka barua ya Mtume Paulo kwa Waefeso, ambamo, Paulo anaonyesha kusifu na kumshukuru Mungu kwa Baraka zake. Ni maombi ya sifa na maelezo ambayo sisi kama waamini wengi hatuna mazoea hayo ya kuianza siku kwa kumtukuza Mungu. Wengi tunaona vigumu lakini kumbe huleta faraja kubwa.

Papa alieleza jinsi sote tunavyojua kusali, tunajua kuomba vizuri sana, hasa kuomba kwa ajili ya mambo yetu binafsi, lakini upande wa kumshukuru Bwana, ni wachache sana wanao fanya hivyo. “Tunashukuru kidogo sana”, Papa alieleza na kuhimiza kwamba, sala za shukurani na Sifa kwa Bwana zinapaswa kuandamana nasi daima.” Kumtukuza Mungu kila wakati, kwa maajabu yake, hasa mambo mengi aliyo yafanya katika maisha yetu, katika Yeye na - katika Kristo, hasa kutuchagua sisi kuwa wana wake hata kabla ya kuumba msingi wa dunia. Tunapaswa kusema, Sifa kwako Bwana, kwa sababu ulinichagua mimi! Ni furaha kubwa kuwa karibu wa Baba.

"Maombi ya sifa" - aliendelea – hutuletea faraja , ni kufurahi mbele ya Bwana. “Tunatakiwa kufanya jitihada za kupata muda wa kuwa mbele ya Bwana na kushukuru. Kumshukuru Mungu kwa kutuchagua. Mungu alinichagua kabla ya msingi wa ulimwengu. Ni jambo tusiloweza kuelewa!

Papa alieleza jinsi ilivyo vigumu kuielewa siri hii ya Mungu , kwamba Bwana alinifahamu mimi hata kabla ya dunia kuumbwa, na kwamba jina langu lilikuwa katika moyo wa Bwana, akisema, hili ni kweli! Huu ni ufunuo! Kama hatuwezi kuamini katika imani ya Kristo, aliongeza, ya kwamba tulitungwa mimba katika asili ya dhambi na kukombolewa kwa damu ya Kristo, basi si Wakristo! Wazo hili huleta furaha kwa mioyo yetu: kwamba “Mimi nimechaguliwa”! Ni mawazo yenye kutupa matumaini. Lakini ili kuelewa hili ni lazima kuingia katika Siri ya Yesu Kristo. Siri ya Mwana wake mpendwa: Yeye aliye mwaga damu yake kwa ajili yetu kwa wingi, kwa hekima na mapenzi yake,, alitekeleza siri ya mapenzi Baba yake.








All the contents on this site are copyrighted ©.