2014-10-17 15:25:28

Mungu ametupa katika mkono wake, ahadi ya Mbingu ya milele- Papa


Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mungu amewapa Wakristo Mbingu kama amana katika umilele. Lakini zawadi hii wakati mwingine hupuuzwa na maisha ya giza la shetani na unafiki. Papa Francisco alieleza katika homilia yake wakati wa Ibada ya Misa, Ijumaa hii , katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican.

Papa alisema, Roho Mtakatifu ni "muhuri" wa mwanga , ambamo Mungu ameitoa mbingu kwa mkono wake kwa Wakristo. Lakini kwa mara nyingi, mwanga huu hugandamizwa chini na uvuli wa maisha yenye gizagiza, mbaya zaidi, unafiki wa kujifanya wajuaji kuliko mwanga wa kweli. Homilia ya Papa Francisco, ilielekeza katika maneno ya Mtume Paulo, kwa Wakristo wa Efeso, ambamo anasema, wanao iamini Injili wamepokea "mhuri wa Roho Mtakatifu. Pamoja na zawadi hii, Papa anasema, Mungu si tu alituchagua kuwapa zawadi ya Roho Mtakatifu, lakini pia katika ubatizo, mnaonyesha mtindo wa njia ya maisha, ambayo ni si kitabia, lakini pia kitambulisho cha Mkristo

Utambulisho wa Mkristo, Papa amesema , hasa ni kuwa na chapa hii ya muhuri wa nguvu ya Roho Mtakatifu, ambayo hutolewa kwa Wakristo wote wakati wa ubatizo. Na Roho Mtakatifu amekwisha piga muhuri wake mioyo ya Wakristo, na kutembea nao. Roho hii, ambaye Yesu aliahidi, si tu hutoa utambulisho, lakini, pia, ni ahadi ya urithi wa Wakristo. Pamoja naye, Wakristo, huanza kuyaonja maisha ya mbingu, hapa duniani, Papa alisisitiza na kuongeza, “ Roho Mtakatifu hutuwezesha kuyaonja maisha haya ya mbingu ya milele, kwa sababu tumepigwa chapa ya muhuri na Roho Mtakatifu, amana ya tuliyowekewa mkononi na Mungu. Tuna Mbinguni kwa mkono wake kwa muhuri huu”.

Lakini, Papa Francisko pia alionya kwamba, kuwa na amana hii, kwa ajili ya Mbingu ya milele haina maana kwamba Wakristo wameondokana na hatari ya kuanguka katika majaribu. Alibainisha, ni wakati ambamo, kama Wakristo, wanapaswa kuzingatia zaidi hatua za kuutafuta utambulisho huu, unaotaka kufunikwa na maisha ya gizagiza na unafiki.
Papa alifafanua maisha hayo ya gizagiza na unafiki akisema, ni maisha ya Ukristo ulio katika joto la uvuguvugu, maisha yasioeleweka, akitolea mfano wa Maisha ya Ukristo wa kwenda tu katika Ibada za Misa siku ya Jumapili, ambayo zaidi ya hilo, hakuna utambulisho mwingine wa kuwa na chapa ya muhuri wa Roho Mtakatifu ndani yake. Na hata wakati mwingine Mkristo huyo huishi kama vile ni Mpagani. Papa Francisco amekemea maisha ya aina hiyo, Ukristo wenye joto la uvuguvugu, yasiyojionyesha sawasawa, akisema huo ni unafiki uliokemewa na Yesu wakati akizungumza na wanafunzi wake, akisema, jihadharini na unafiki wa Mafarisayo. Na ndivyo pia sisi tunaojiita Wakristo, tunaweza kufanana nao , kujifanya kuwa Wakristo lakini kumbe kwa ndani siyo. Watu tusiosema ukweli wa mambo yaliyo ndani mwetu.

Papa ametaja Ukristo wa kweli, uliopigwa muhuri wa Roho Mtakatifu ni maisha yenye Upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kujizuia kutenda dhambi. “Hiyo ndiyo njia yetu ya mbinguni, ni barabara yetu, ambayo huianza Mbingu hapa duniani” Kwa muhuri na Roho Mtakatifu, tunakuwa na kitambulisho kinachotupa amana ya kuyaishi maisha ya kimbingu” Papa alikamilisha kwa kumwomba Bwana, neema ya kuwa makini na muhuri huu, Utambulisho wetu cha Kikristo, ambayo ni si tu ahadi, hakuna, sisi tayari tuna amana hiyo mkononi.








All the contents on this site are copyrighted ©.