2014-10-15 08:33:33

Siku ya kunawa mikono duniani!


Jumuiya ya Kimataifa, Jumatano tarehe 15 Oktoba 2014 inaadhimisha Siku ya Kunawa Mikono Kimtaifa, changamoto iliyotolewa na Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, ili kuokoa maisha ya watoto chini ya miaka mitano wanaofariki dunia kutokana na magonjwa ya kuhara.

UNICEF inasema magonjwa ya kuhara kwa watoto ni chanzo kikubwa kwa watoto hao kudumaa, mambo yanayosababisha madhara makubwa kwa ustawi na maendeleo ya kiuchumi. Tabia na utamaduni wa kunawa mikono kila wakati ni mchakato unaoweza kuwakinga watoto wadogo dhidi ya magonjwa ya kuhara.

Ni kitendo cha kawaida kabisa kunawa mikono kwa sabuni, lakini kina maana kubwa kwani kinaweza kuokoa maisha ya watoto ambao ni tegemeo kubwa la taifa. Watoto wadogo waelimishwe umuhimu wa kunawa mikono kabla na baada ya kula na wakati wote wanapomaliza kujisaidia. Watoto wakijengewa tabia ya kunawa mikono, wataweza kuimarisha afya zao kwa kujikinga na magonjwa ya kuhara ambayo yamekuwa ni chanzo kikubwa cha vifo vingi vya watoto duniani.









All the contents on this site are copyrighted ©.