2014-10-15 15:10:14

Sala ya Papa Francisko kwa wote wanaoteseka!


Kuna watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaendelea kuteseka kiroho na kimwili. Hawa ni watu ambao wanakumbana na vita, njaa, umaskini, magonjwa pamoja na majanga asilia. Myumbo wa uchumi kimataifa umepelekea watu wengi kukosa fursa za ajira, kukosa uwezo wa kuhudumia familia zao na pengine hata kukata tamaa.

Yote haya ni mahangaiko yanayogusa maelfu ya watu duniani! Kuna watu pia wanaendelea kunyanyaswa na kudhulumiwa kutokana na misimamo mikali ya kiimani; watu wanateseka kutokana na kinzani na misigano ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anamwomba Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji watu wote wanaoteseka hususan wagonjwa, watu wenye shida na mahangaiko mbali mbali pamoja na watu wasiokuwa na fursa za ajira.









All the contents on this site are copyrighted ©.