Zaidi ya wananchi millioni kumi kutoka Msumbiji, Jumatano tarehe 15 Oktoba 2014 wanashiriki
katika uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge. Chama cha Frelimo kinakabiliwa na ushindani
mkubwa kutoka kwa Chama cha Renamo kinachoongozwa na Bwana Alfonso Dhlakama. Bendera
ya Frelimo katika uchaguzi wa mwaka 2014 inapeperushwa na Bwana Filipe Nyusi aliyekuwa
Waziri wa ulinzi. Frelimo kimekuwepo madarakani, tangu Msumbiji ilipojipatia uhuru
wake kunako mwaka 1975.
Ni matumaini ya wananchi wa Msumbiji kwamba, viongozi
watakaochaguliwa watajikita zaidi katika kutafuta mbinu mkakati wa kuibua fursa za
ajira pamoja na kuwa na mgawanyo bora zaidi wa rasilimali na fursa za kiuchumi zilizomo
nchini humo. Watu wanatarajia kwamba, Msumbiji inaweza kuibuka kidedea katika masuala
ya kiuchumi licha ya kinzani za kisiasa na majanga asilia yanayokwamisha juhudi hizi.