2014-10-14 10:08:17

Wananchi wana wasi wasi wa afya ya Rais Sata wa Zambia


Vyama vya kijamii nchini Zambia katika taarifa yake vinaonesha wasi wasi wao kuhusu afya ya Rais Michael Sata baada ya kutoonekana hadharani kwa kipindi kirefu. hali hii imepelekea vyombo vya habari vya kimataifa kuzungumzia kwamba, Rais Sata kwa sasa anakabiliwa na hali tete ya afya. Rais Sata hivi karibuni alishindwa kuhutubia Bunge la Zambia kutokana na sababu za kiafya, mambo ambayo yanaongeza wasi wasi kwa wananchi wengi wa Zambia.

Wachunguzi wa mambo wanasema, tarehe 19 Septemba 2014, Rais Sata alilazimika kufupisha hotuba yake na hivyo kuwaacha watu wengi wakiwa wameshikwa na bumbuwazi. Hadi leo hii wananchi wa Zambia hawajapata majibu sahihi kuhusu afya ya Rais Michael Sata. Vyama vya kiraia vinaliomba Bunge kuunda tume maalum ili kuchunguza afya Rais Sata au vinginevyo, Rais aendelee kutekeleza wajibu wake barabara ili kuwahakikishia wananchi wa Zambia kwamba, yuko "ngangari".







All the contents on this site are copyrighted ©.