2014-10-13 10:20:53

Waziri mkuu wa Vietnam kukutana na Papa Francisko


Baba Mtakatifu Francisko, anatarajiwa Jumamosi tarehe 18 Oktoba, majira ya mchana, kukutana na kuzungumza na Waziri mkuu Nguyen Tan Dung wa Vietnam. Taarifa hii imetolewa na Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican na kufafanua kwamba, hii itakuwa ni fursa makini kwa Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake kufanya upembuzi yakinifu kuhusu mahusiano kati ya Vietnam na Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.