2014-10-13 16:19:25

Sinodi Maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia yaanza kipindi cha pili


Sinodi Maalum ya Maaskofu kwa ajili ya familia, imeanza awamu ya pili ya majadiliano. Mababa wa Sinodi, katika wiki hii , ambayo ni wiki ya mwisho ya majadiliano, pamoja na vikao, pia wamegawanyika katika vikundi vidogovidogo kwa ajili ya majadiliano ya kina michango iliyotolewa.

Kardinali André Vingt Trois: akirejea kipindi cha kwanza cha sinodi, ameeleza kwamba, wajumbe wote waliweza walipata fursa kusema bila hofu, kama Papa Francisko alivyoomba tangu mwanzo wa Sinodi hii, Mababa wa Sinodi kusema ukweli, bila woga, na kusikiliza shuhuda kwa unyenyekevu, na kwa moyo wazi.

Kardinali Trois, amekuwa na imani kwamba, awamu ya kwanza ya vikao vya Sinodi, imetoa ukweli wa hali halisi katika maisha ya ndoa na familia katika mtazamo wa Kanisa, kutokana na vikao kufanyika katika mazingira ya kusema ukweli bila hofu na kusikiliza wengine kwa makini, kama Papa Francisco aliyewaita, kusisitiza na kuwatia moyo. Na ndivyo ilivyokuwa hali na tabia ya vikao katika awamu ya kwanza, waliweza kusikiliza maelezo na maoni mbalimbali, kwa ajili ya kuweza kujua misingi ya hali katika Mabaraza ya Kiaskofu.

Na kwamba , uhuru huu ni kipengele muhimu katika umoja wa Sinodi, kama Papa Paulo VI, alivyounda mfumo huu wa sinodi karibia miaka 40 iliyopita. Mfumo huu uliundwa ndani ya Kanisa kwa ajili ya kupata mtindo wa Kanisa kufikia maamuzi ya utekelezaji wa kazi za Kanisa katika ulimwengu huu.

Kardinali Andrè Vingt, pia amezungumzia juu ya changamoto ya Kichungaji ndani ya familia, kwa kutoa maoni yake binafsi kwamba, pamoja na kuwa na masuala mengi yanayofanana pia sinodi, imewasaidia kuona kwamba, kuna kutofautiana katika changamoto hizi. Wameona kwa mfano, wasiwasi wa kichungaji kwa nchi za Magharibi Ulaya au dunia ya Magharibi, si sawa wasiwasi walio nao Maaskofu kutoka nchi za Kusini. Na hivyo katika maamuzi ya mwisho ni lazima, mkazo uzingatie pia ujumla wa Kanisa la Ulimwengu, si tu katika kutazama changamoto zilizo upande fulani wa dunia, mfano matatizo yaliyomo katika nchi za Ulaya ya Magharibi. Ni lazima kuwa makini katika kutolea majibu ya kupambana na changamoto, katika muono kwamba, tatizo la Ulaya si tatizo kwa nchi za Asia au Afrika. Ametoa mfano mwingine kuwa katika nchi nyingi za Asia, wanawake hulazimika kuondoka kwenda kutafuta fedha kwa ajili ya familia zao, tatizo ambalo kwa nchi za Magharibi halipo. Au matatizo ya wanawake wengi wa Kiafrika kuzaa watoto wengi bila kuwa na mme wa ndoa, hivyo hulazimika kulea na kusomesha watoto wao wenyewe bila msaada wa bwana aliyezaa nae. Hili ni tatizo kwa wanawake wengi wahamiaji pia , ambao hulazimika wakati mwingine kuwa mbali na watoto wao, ni sehemu ya changamoto za Kanisa katika nchi nyingi , hasa Asia na Afrika, aliongeza.








All the contents on this site are copyrighted ©.