Mateka 27 wa Boko Haram waachiliwa huru nchini Cameroon
Rais Paul Biya wa Cameroon, mwishoni mwa juma ametangaza kwamba, Kikundi cha Boko
Haram kimewaachia huru mateka ishirini na saba waliokuwa wametekwa hivi karibuni,
Kaskazini mwa Cameroon. Watu hawa walitekwa nyara kunako tarehe 16 Mei huko Waza na
tarehe 27 Julai huko Kolofata, maeneo ambayo yako Kaskazini mwa Cameroon na mpakani
na Nigeria.
Wachunguzi wa mambo wanabainisha kwamba, pengine hata wale wanafunzi
wasichana waliotekwa nyara huko Chibok, Nigeria wako katika eneo hili. Rais Biya akizungumza
kwenye Radio ya taifa amefafanua kwamba, watu walioachaliwa huru wako salama, ingawa
hakukupatikana ufafanuzi zaidi. Mateka hawa wameachiliwa huru wakati Jumuiya ya Kimataifa
ikiendelea kushutumiwa kwa kutolivalia njuga tatizo la Boko Haram, wanaoendelea kuhatarisha
amani na usalama Kaskazini mwa Afrika.