Kanisa Katoliki Kenya lakosoa kampeni ya chanjo ya pepopunda kwa wanawake
Tume ya Afya ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya , ina mashaka na kampeni ya chanjo
ya pepopunda inayolenga kutolewa kwa wanawake walio katika umri kati ya miaka 19-49,
umri wa uzazi , ambayo itaanza wiki ijayo kama ilivyoandaliwa na Wizara ya Afya Kenya.
Kanisa lina mashaka na mpango, ulioitwa kama ni mpango wa siri wa serikali, unaolenga
kufanya wanawake wengi kuwa wagumba wanawake, kama hatua ya kudhibiti idadi ya
watu.
Tamko hilo limenukuliwa na vyombo vya habari, kama lilivyotolewa na Tume
ya Afya ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya katika mkutano wa hivi karibuni uliofanyika
katika Kituo cha Kichungaji cha Mtakatifu Patrick cha Kabula Bugoma . Tmko hilo lilitiwa
sahihi Wenyekiti wa Tume Katoliki ya Afya Kenya, Askofu Paul Kariuki Njiru wa Embu
na , Askofu Joseph Mbatia wa Nyahururu , kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki
Kenya . Tume hii ni pamoja na wasimamizi wa vituo 24 vya Afya vya majimbo Katoliki.
Tume
imeilalamikia Wizara ya Afya, kuandaa kampeni hii ya chanjo kichinichini bila kuutangazia
wazi umma sababu na athari za chanjo ya pepopunda. Na wametaka kujua kwa nini tangu
mwanzo chanjo ya pepopunda haikuingizwa katika kampeni ya Shirika la Afya la Dunia
WHO, chanjo dhidi ya polio na malaria.
"Tunataka kujua kama kuna mgogoro
katika pepopunda Kenya, na kama ndivyo, kwa nini haikutangazwa waziwazi? Na kwa nini
inalenga tu wanawake walio katika umri wa kuzaa, umri wa kati ya miaka 19-49; na kwa
nini imewaacha nje wasichana wadogo, wavulana na wanaume iwapo wote wanaweza kukabiliwa
na ugonjwa wa pepopunda? Na miongoni mwa magonjwa mengi yanayotishia maisha ya watu
Kenya, kwa nini pepopunda imepewa kipaumbele? " Ni maswali yaliyoulizwa na viongozi
wa kidini, walipokutana na waandishi wa habari katika Kituo cha Kichungaji cha Mtakatifu
Patrick katika Kitongoji cha Kabula, Bungoma.
Naye Mkurugenzi wa huduma
za tiba, Dr Nicholas Muraguri, akirejea upinzani huu amesema, hakuna sababu za kuwa
na hofu juu ya chanjo ya pepopunda, i kwa kuwa ni kati ya chanjo msingi za kawaida,
ambayo hutolewa kwa mama wajawazito wote nchini kote Kenya na kama ilivyo duniani
kote. Na kwamba hawana tatizo na Kanisa na hivyo Mkuu wa kitengo cha Chanjo, Ephantus
Maree anapanga kukutana na viongozi wa kanisa hivi karibuni, kuelezea umuhimu wa chanjo
hiyo..
Pepopunda ni miongoni mwa magonjwa mengi ya kawaida, yenye kuwa na
matokeo mabaya kwa wmama ya wanaojifungua hasa katika mazingira mchafu na wenye
mazoea ya kufunga kitovu cha mtoto kwa kutumia njia asilia kama kufunga kwa kamba,
na mzazi akipatwa na vijidudu vinavyo sababisha pepo punda anakuwa katika hatari ya
kifo kwa asilimia 100 kama hakuwahi kutibiwa.
Dr Maree anasema , Kenya
ni miongoni mwa nchi 28 duniani ambazo bado kutokomeza ugonjwa wa pepopunda, tangu
WHO ianzishe kampeni yake mwaka 1989 kwa lengo la kufuta ugonjwa huo duniani ifikapo
mwaka 1995. Kenya bado upo na hivyo serikali imeweka mkazo zaidi katika wilaya zake
60, hasa vitongoji 16 ambako ugonjwa pepopunda bado ni tishio la maisha.
Nalo
Kanisa linasema, linataka serikali itoe taarifa za kutosha, ili umma kwa ujumla
uelimishwe kwa lengo la kuepuka taarifa potofu na propaganda kuhusiana na chanjo
hiyo, na heshima ya binadamu katika maisha na huduma za afya za lazima kama kipaumbele.