Papa: Mungu baba anatupatia zawadi kubwa ya Roho Mtakatifu:
Katika sala tunaomba mambo mengi lakini zawadi kubwa tunayoweza kupokea ni Roho Mtakatifu.
Ni maneno ya Papa Francisko katika Homilia yake Alhamisi 9 Okotaba katika Kanisa
dogo la Mtakatifu Marta Vatikan. Akitafakari juu ya Injli ya siku iliyokuwa ikimwonyesha
mwanaume mmoja aliyekwenda usiku wa manane kwa rafiki yake ili apate kusikilizwa ombi
lake.
Papa alisema, Mungu ana huruma, siyo kwamba anasamehe tu ,bali yeye ni
mwema anatupatia zaidi ya kile tuombacho. Ni kwa sababu aliongeza, daima sisi tunaomba
hiki na kile, na Mungu daima anatoa.
Alielendelea, katika Injili ilionyesha
vitu vitatu, rafiki, baba na zawadi, kwa namna hiyo Yesu aliwaonyesha mitume namna
ya kusali kupitia mfano wa mwanaume aliyekwenda usiku wa manane kwa rafiki yake kuomba
chochote. Aliongeza kwamba, katika maisha kuna marafiki wema, ambao kiukweli hutoa
kila kitu, lakini vilevile kuna hata wengine ambao ni wema hivihivi tu, kwa maana
hata Biblia inasema kwamba, wapo wawili au watatu na siyo zaidi. Wengine ni marafiki
lakini siyo kama hawa, maana wanatoa kadiri ulivyoomba.
Injili inaeleza, Papa
aliongeza, kwamba Yesu aliweza kusema kwamba ni baba yupi kati yetu ambaye mtoto atomwomba
samaki, na badala ya samaki apewe nyoka, au kuomba yai na apewa nge? Kama nyingi mliyo
katili mnaweza kuwapatia kilichochema watoto wenu, ni jinsi gani Baba aliye mbinguni?
Aliendelea,
siyo rafiki peke yake anayetusindikiza katika safari ya maisha, na kutupatia kile
tunachokihitaji, bali yupo hata Baba wa mbinguni anayetupenda sana ambaye Yesu alisema
kwamba anahangaikia hata ndege wa angani wapate chakula. Yesu anataka kuhamasisha
imani katika sala, na anasema ombeni, mtapewa, tafuteni mtapewa, na bisheni mtafunguliwa
kwahiyo Papa Francisco aliongeza, kuomba na kutafuta ni sawasawa na kubisha hodi katika
moyo wa Mungu. Na Mungu atawapatia Roho Mtakatifu wote ambao wanaomuomba.
Hiyo
ni zawadi kubwa ya Mungu, kwani Mungu hawezi kukupatia zawadi ambayo hukuomba vizuri
na iwapo zawadi haina manufaa kwako. Lakini Bwana anatupatia zaidi Roho Mtakatifu,
ambayo ndiyo zawadi ya kweli , na ambayo nafsi zetu hazijui kuomba. Alimalizia
Papa akisema sala lazima zinafanyika pamoja na rafiki, ambaye ndiye msindikizaji wa
safari ya maisha,ifanyike kwa njia ya baba wa mbinguni na Roho Mtakatifu na rafiki
Yesu.
Yesu anatusindikiza na anatufundisha kusali. Na sala yetu inapaswa kufanyika
kwa njia ya Utatu Mtakatifu. Aliuliza kama wengine wanaamini, na kujibu ndiyo, na
kama wanaamini Mungu, Je ni nani kwao?
Na kwa wengine wanaosema kuwa Mungu
hayupo , aliwaonya kwamba wasikufuru kwa sababu Mungu yupo, Mungu Baba, mwana na Roho
Mtakatifu yupo. Yesu anatusindikiza katika safari na kutupatia kile tuombacho;na Baba
anatutunza na kutupenda, na pia kutuzawadia Roho Mtakatifu ambayo ni zawadi kubwa
zaIdi.