2014-10-09 16:39:28

Sinodi: Michango Kard. Erdo , Kardinal Sistach


Mapendekezo ya Kardinali Peter Erdo :Kutazama familia kwa matumaini na Huruma

Familia siyo mtindo uliyopitwa na wakati, kinyume chake, Kanisa, linaendelea kuiona familia kuwa chimbuko la matumaini na hurum, na hivyo ndoa haziwezi kutenganishwa kiholela. Pale inapobidi kutenganisha ndoa, basi ni lazima kufuata kanuni na mwongozo wazi wa hali halisi ya familia. Ni Kutazama familia kwa matumaini na huruma , na kutangaza thamani na uzuri wake pamoja na matatizo mengi yanayoweza kuikabili.

Kardinali Peter Erdo, Askofu Mkuu wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya Mashariki, alieleza katika mahojiano na wanahabari baada ya Papa, kuihutubia Sinodi siku ya Jumatatu, wakati wa kuanza kwa Kazi ya Sinodi.

Kardinali Erdo alisema kwamba, tunaishi dunia iliyojaa mshituko na wasiwasi , maisha yasiyo mpanglio, yaliyo geuzwa kuwa na vipindi vingi, hali ya sasa inaogopesha ambapo binadamu amejazwa na ubinafsi. Lakini kwamba kipindi hiki cha sasa mbele ya ishara za nyakati, Injili ya familia inawezekana kufanya mageuzi, maana Injili ni dawa ya kweli, ambayo inaweza kuhamasisha hasa waliosahaulika pembezoni mwa jamii, wale ambao wanapata shida ya kutambua namna ya kuishi.

Kuhusu tatizo la kutenganisah ndoa na Sakaramenti yake kati ya wabatizwa Kardinali Erdò anasema kwamba, inabidi kuwepo na mafundisho thabiti kati ya wachumba ili wapate kuelewa hadhi ya sakramenti ya ndoa, umoja wa wanandoa , maana ya uaminifu na mafanikio yao, katika taassisi ya jamii. Hata kama ndoa inatishiwa na usumbufu kama ule wa talaka, utoaji mimba, vurugu, umasikini , unyanyasaji , na jamii kukosa ulinzi na usalama,vilevile matatizo ya uhamiaji, bado ina thamani kubwa kwa mmungano halali wa mke na mme .

Kardinali aliendela kwamba hakuna kuhama au kujiuzulu ndani ya Kanisa maana kuna urithi mpana wa Imani na katika kushirikishana. Na aliizungumzia hali ya sasa ya aina za kiitikadi kama vile nadharia ya usawa wa kijinsia , au muungano wa ndoa ya mashoga kati ya mwanaume kwa mwanaume au kati mwanawake, ambayo haikubaliki kwa Imani ya Kanisa Katoliki ambalo bado linaendelea kuiona ndoa na familia kwamba bado ndiyo urithi wa binadamu, unaotakiwa kudumishwa, kuhifadhwa, kukuzwa na kulindwa.

Kardinali akiongea juu ya mafundisho ya kanisa akisema kwamba Ni dhahiri waamini wengi wamezembea katika mafundisho ya Kanisa lakini haina maana kwamba haiwezekani kujadili.

Pamoja na Matatitizo hayo yanayokabili familia na hasa kwa upande wa uchumi na tekolojia, Kanisa linazidi kutoa misaada ya kweli hata kama misaada hiyo haiwezekani kutosheleza kuchangia juhudi za nchi husika katika kuhamasisha na kukuza manufaa ya watu wote kwanjia ya siasa inayofaa.

Na aliitazama huruma ya Kanisa kwa wanandoa na kusema kwamba, inabidi kuangalia ni nani mwenye makosa , na aliyevunja ndoa hiyo ni nani. Lakini kazi ya kichungaji ya Kanisa inapaswa kuwasadia watu hawa, wale waliopata talaka na kuoelewa ndoa ya kiserikali kwasababu wako ndani ya Kanisa.Wanahitaji msaada na na wanayo haki ya kusindikizwa kichungaji..

Pia Kardinali katika mapendekezo yake juu ya Injili ya maisha na hasa kwa upande wa kupokea maisha katika maisha ya wenye ndoa kutokana na mitindo ya kisasa, alisema kwamba wengi wamecha gua kutokuwa na watoto na wengine kutaka kutafuta watoto kwa kila njia. Aliongeza kwamba familia hizo zinapaswa pia zisindikizwe , kwani mara nyingi familia zimeachwa peke kiupweke na ndipo majanga makubwa yamejitokeza na kusikia yowe na mateso ambayo yangeweza kuzuliwa mapema.

Na mwisho Kardinali alisema kwamba, Sinodi hii inachangmoto kubwa na hasa ya kuweza kuzingatia hali ngumu ya dunia na hasa mzunguko wa wakatoliki na kufikiria hali zao za kijamii kwa namna ya kuhamsisha ujumbe wa kikiristo juu ya ndoa na familia, na kuweza kutoa jibu la kweli liliojaa upendo, kwani dunia inahitahiji Kristo

Kardinali Sistach Lluís Martínez Sistach, Askofu Mkuu wa Barcelona (Spagna): Kanisa lipo kwaajili ya uinjilishaji.
Akiojiwa na mwandishi wa habari wa Radio Vatican Paolo Ondarza, kuhusu Sinodi hii juu ya familia alisema kwamba wao wanataka kuonyesha uzuri wa ndoa na wa familia ambao ndiyo kiini cha jumuia ya maisha ya upendo, na hivyo mada msingi ya familia ni muhimu.

Kama Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican usemavyo ,“wema wa mtu na wa jamii ya binadamu na mkristo, kwa maana ya jamii na ya Kanisa , hutegemea sana familia" inabidi kufanya kazi ya kufundisha vijana kwani wanapooana wajue kwamba upendo wao umekomaa na ni katika maisha yote kuwa waaminifu na kutoa matunda.

Karidnali aliongeza kueleza juu ya mafundisho ya kanisa juu ya ndoa na familia akisema kwamba anafikiri mafundisho ya kanisa ni mengi , lakini mafundisho hayo yanakutana na vigezo vingi kama vile watu hawana muda wa kusoma, kujifunza na kuskiliza. Lakini Kanisa lina utajiri mkubwa wa kutoa mafundisho juu ya upendo kwa maisha yote, ya kushirikishana katika kupokea maisha, elimu ya maisha ya kikristo na watoto, na haya mafundisho yanatoa furaha kwa watu wote.

Alitoa mfano akisema, hivi karibuni aliadhimisha Misa ya familia moja ilIyokuwa inaadhimisha mwaka wa 50 wa ndoa , ushuhuda wa ndoa hii ni ujumbe kwa vijana wote,kuonyesha juhudi ambazo daima zinapaswa kutendeka katika kuishi maisha yote ya ndoa bila kutengana na ndoa ni jambo lisilo tenganishwa. Japo maisha ya ndoa siyo rahisi lakini wapo watu wa kusaidia kuyakamilisha .

André Vingt-Trois, Askofu Mkuu wa Paris : ugumu wa kupokea mafundisho ya Kanisa.
Jumatatu 6 Oktoba mchana katika Sinodi inayoendelea ikiongozwa na Mwenyekiti mjumbe, André Vingt-Trois, Askofu Mkuu wa Paris , katika utangulizi wake, uliangalia juu ya muhtasari wa kikao cha maandalizi ya Sinodi au miongozo ( Instrumentum laboris) juu ya mpango wa Mungu kwa ndoa na familia (Sehemu I, 1) Maarifa na Kukubali Mafundisho juu ya Ndoa na familia kutokana na Maandiko Matakatifu na Nyaraka (Sehemu ya I, 2)

Kardinali alibainisha kuwa hata kama Kanisa linafundisha juu ya ndoa na familia inajulikana kwamba wakristo wengi wanakuwa na ugumu kikamilifu wa kupokea mafundisho hayo na hivyo inabidi wachungaji kuanza upya wa mafundisho ya ukweli wa Imani ambayo ndiyo uwezekeno wa kulinda binadamu na thamani yake. .
Vilevile aliwakaribisha wanandoa waliochaguliwa na Mababa wa Sinodi kuelezea hali halisi ya maisha ya ndoa, ambao ni Romano na Mavis Pirola ambao wameishi ndoa kwa miaka 55 ni wazazi wa watoto wa 5 wakiwa na wajukuu 8. Wote wawili ni wakurugenzi wa chama katoliki cha ndoa nchini Australia

Waliliambia sinodi kwamba maisha ya familia ni huruma, lakini zaidi ni maisha ya kiparokia, ambayo ni familia ndani ya familia, wao pia waliwasilisha pia hali ya wakatoliki ambao wamepata uzoefu wa kuvunja ndoa na mivutano kati ya maisha yao, na wakati huohuo wakitaka kuendelea kufuata mafundisho ya kanisa.
Walitoa mfano wa mama mmoja aliyepata talaka na akakosa kupokelewa mtoto wake kanisani, au wazazi waliotakataa watoto wao mashoga wasipeleke wapenzi wao nyumbani wakati wa sikukuu ya noeli , vilvevile mwanamke mjane ambaye anamlea mtoto mlemavu.

Wanandoa hao walisema kwamba kanisa daima linakabiliwa na mvutano wa ukweli wakati likielezea juu ya huruma na msamaha. Lakini inawezekana kufaidika kwa kufundishwa na mapingo ya kimaisha , na zaidi ya yote, Kanisa linahitaji kuwasindikizia katika safari yao kwa kuwakaribisha na kusikiliza historia zao.








All the contents on this site are copyrighted ©.