Papa Francisco katika katekesi yake Jumatano 8Oktoba katika uwanja wa Kanisa Kuu
la Mtakatifu Petro, Vatikan, amegusia juu ya Wakristo wasiyokuwa Wakatoliki, akisema
kwamba katekesi zilizopita alijaribu kuweka mwanga wa asili na uzuri wa Kanisa, na
kujiuliza ni kitu gani kinafanya mtu awe mmojawapo wa watu wa Mungu ambao ni Kanisa.
Inabidi
lakini tusisahau kwamba kuna wengine wanashiriki imani ya Kristo na Wakatoliki japokuwa
siyo Wakatoliki bali ni wa madhehebu mengine, au wenye kuwa na kanuni tofauti na Wakatoliki.
Papa
alibainisha kwamba wengi wamegawanyika na hata ndani ya Kanisa Katoliki,mgawanyiko
huu unatokana na historia ya vurugu , mateso, na hata vita . Papa alisema hii ni aibu!
Alikiri hata leo mahusiano siyo mazuri. Na kisha kuhoji, je sisi tunajiweka katika
hali gani juu ya hilo jambo? Je na sisi tumejiachia au tunaamini kikamilifu kwamba
tunapaswa kutembea pamoja kwenye mwelekeo wa mapatano na muungano kamili ? Ni muungano
kamili wa kuweza kushiriki wote pamoja katika mwili na damu ya Yesu. Mgawanyiko
wa Wakristo, aliendelea , ukiumiza Kanisa, humumiza Kristo, pia na sisi tunapotengana
tunamumiza Kristo: Kanisa kwa hakika ni mwili ambao Kristo ndiye Kiongozi. Papa alibainisha
; mnajua wazi ni jinsi gani umoja ulikuwa moyoni mwake Yesu kwa mitume wake alipowaeleza
wabaki na umoja katika upendo wake. Inatosha tu kufikiria maneno yake kutoka Injili
ya Mtakatifu Yohana, ambayo ni sala ikimwelekea Baba yake kabla ya mateso, na kusema
“ Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulionipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi
tulivyo (Yn 17,11)”.
Umoja huo ulikuwa tayari uko hatarini wakati Yesu yupo
kati ya watu wake, aliendelea Papa kwamba, kwani katika Injili inaonyesha mitume wakijalidiliana
ni nani atakuwa mkubwa kati yao. (cfr Lc 9,46)Bwana alikazia lakini juu ya umoja
kwa jina lake Baba , akitaka watambue kwamba ushuhuda wao uwe wa ukweli ambao utaweza
kuleta muungano na kutakiana mema, kwa hiyo mitume baadaye walitambua hadi Mtakatifu
Paulo akafika na kuiambia Jumuiya wa Wakorinto kwa maneno haya: Basi ndugu nawasihi
, kwa jina la Bwana wetu Yesu kristo , kwamba nyote mnene mamoja, wala pasiwe kwenu
faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja(1 Kor 1,10)”.
Papa aliongeza
kwamba ni uchungu mwingi kwa mgawanyiko uliopo kati ya wakristo, tumegawanyika kati
yetu, na wakati huo kuna jambo linalotuunganisha ambalo, wote tuaamni Yesu Kristo
Bwana, wote tunaamini katika Baba , Mwana na Roho Mtakatifu na tatu wote tunatembea
pamoja maana tupo safarini. Tunapaswa kusaidiana aliongeza Papa. Pamoja na kuwa katika
jumuiya, kuna watu wenye akili, kuna wanatelojia wanaotafuta ukweli, kwa sababu ni
lazima, lakini wote inabidi kutembea kwa pamoja.
Njia hii inayoitwa ya kiekumeni,
ya kiroho ni kutembea njia ya maisha pamoja katika imani yetu ndani ya Bwana Yesu
Kristo. Katika Katekesi hii, Papa pia alikumbuka tukio lake mwenyewe la miaka
70 iliyopita, siku alipopokea kumunio ya kwanza, akieleza kwamba, kupata kumunio
ya kwanza inabidi kila mmoja kutambua kuwa ni kufanya muungano wa ndugu wote wanao
amini Yesu na wale wa kutoka madhehebu mengine. Alimalizia Katekesi yake akisema,
twende mbele tukitafuta ukamilifu wa umoja, pamoja na kwamba historia ilitutenganisha,
lakini bado tupo safarini kuelekea mapatano na muungano. Huu ni kweli , na wote inabidi
kutetea safari ya muungano. Tunapojisikia kukata tamaa na safari kuwa ndefu bila kufika
, tukumbuke kwamba, Mungu hawezi kufunga masikio dhidi ya sauti ya Mwana wake Yesu
anayesikiliza sala zetu ili Wakristo wote kweli wanakuwa kitu kimoja.