2014-10-07 15:13:21

Papa afungua Sinodi:Ongeeni kwa uwazi, msiwe na woga.


Jumatatu 6 Oktoba Papa katika hotuba yake ya ufunguzi wa Sinodi , aliwasalimia washiriki wote wa Sinodi hii juu ya Familia, iliyoanza Jumapili kwa adhimisho la Misa Takatifu. ALIwashukuru kwa juhudu kubwa ya kuandaa tukio hilo. Alitaja kwamba wahusika wa maandandalizi wamekuwa na subiri ,na umakini kwa miezi mingi wakiwa wanasoma na kutafakari juu ya Sindodi hii.

Papa alimshukuru kwa namna ya pekee kardinali Lorenzo Baldisseri Katibu Mkuu na kaimu wa Sinodi Monsinyo Fabene Fabio, na wote walioshiriki kwa kwa ujumla kuandaa.

Aliwashukuru Makardinali, MapatriakI, Maaskofu, Mapadre, Watawa wake kwa waume , na Walei, kwa uwepo wao ambao ni utajiri wa kuimarisha kazi ya roho ya Mama wa sinodi, kwa ajili wa manufaa ya kanisa na familia. , Alibainisha kwamba uwepo wa watu hawa ni pendekezo la roho ya kazi ya Sekretarieti na wajumbe wenyeviti wa Sinodi maalumu.

Papa alitaja kwamba , kwanza walichaguliwa kabla ya mkutano wa Sinodi na pia kuchaguliwa na washiriki wa Mkutano wa mwisho wa Sinodi. Papa alisema , kwa kuwa kazi ya kuchagua ilipaswa kufanywa na yeye , basi, aliomba ushauri wa pendekezo kutoka kwa wajumbe kabla ya Sinodi, na kuwataja wale ambao kamati ilikuwa imewapendekeza.

Papa aliendelea, wao wanawakilisha sauti ya Kanisa kutoka katika mkusanyiko wa Baraza katoliki la maaskofu. Na Kanisa mahalia ni taasisi za binadamu; kwamba sauti yao wataiwakilisha katika sinodi. Alibainisha kuwa; ni wajibu mkubwa, kwa sababu wanawakilisha matatizo ya Kanisa, ili lipate kutembea katika njia ya injili. Kwa kufanya hivyo Papa aliwashauri kwamba, jambo msingi ni kuongea wazi ,na kwamba hakuna mtu kufikiri nikiongea nitafikiriwa hivi au vile. Ni lazima kukiongea wazi kile ambacho unajisikia kuongea kutoka rohoni Papa aliwasisitiza wajumbe.

Alitoa mfano wa ripoti ya mwisho wa Mkutano wa mwisho wa Februari 2014 juu ya familia, Kardinali aliandika kwamba baadhi ya Makardinali hawakupata ujasiri wa kusema jambo juu ya Papa, wakifikiri kwamba Papa atawafikiria vibaya. Papa ametaja woga wa namna hiyo ni makosa. Siyo vizuri, kwa kuwa hiyo si maana ya kuwepo katika sinodi, kwa sababu inabidi kuongea ambacho katika roho wa Bwana unacho jisikia kusema. Bila kujali heshima ya cheo cha binadamu, na bila woga, wakati huo inabidi pia kusikiliza kwa unyenyekevu , na kupokea kwa moyo wazi yale ambayo wengine wasema. Papa aliongeza.

Papa alirudia akiwataka ndugu hawa kuongea wazi na kusikiliza kwa unyenyekevu: wafanye hivyo kwa utulivu na amani kwa sababu Sinodi imekuwepo kwa njia ya Petro na ndani ya Petro na uwepo wa Papa ni udhamini kwa wote na ulinzi wa imani.

Alimalizia hotuba kwamba, wote washiriki kwa pamoja ili kutoa ufumbuzi wazi wa safari ya Sinodi hiyo. Na Bwana Yesu Mwana wa Familia ya Nazareth, awaangazie kwa njia ya Roho Mtakatifu, kuishi na kufuata matashi ya Baba; na katika njia ya uwepo wake, abariki matunda ya kazi na nguvu zao ili , wafunguke mioyo na njia zao ambazo kibiubindamu hazitarajiwi.

Kardinali Bardisseri:
Kardinali Bardisseri Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, alitoa hotuba ya utangulizi wa Sinodi Jumatatu 6,2014 , na salaam maalum za kwanza kama Katibu Mkuu wa Sinodi maalumu ya Maaskofu tangu alipoteuiwana papa Fransiscco21 Septemba 2013. Alimshukuru Papa kwa maamuzi yake ya kufanya Sinodi hii, ikiwa mwanzoni kabisa mwa shughuli yake ya kichungaji,kwa Madambiu:Changamoto za kichungaji juu ya Familia katika Mantiki ya Uinjilishaji.

Kardinali aliendelea, kwa kurejea homilia ya kwanza ya Papa, aliyoitoa katika Kanisa Dogo la Sistina, 14 Machi 2014,ambamo alitamka maneno matatu: kutembea, kujenga na kukiri, akiweka kutembea iwe nafasi ya kwanza .

Kutembea kwa Pamoja ndiyo imekuwa hatua ya mwanzo kabla ya Sinodi, Ni Kanisa ambalo ni Jumuiya za Waamini katika Kristo, wanatembea pamoja , kuelekea nyumbani kwa Baba, ni utume wake duniani, kwenda kutangaza na kukiri imani ya Yesu Kristo, kwa njia ya karama mbambali za Kanisa na huduma, ambazo zinaunganisha na kutoa ushuhuda wa Injili.

Na aliongeza na kushukuru kwa habari njema na neema kwa Kanisa, kwamba, Sinodi na Kanisa zima linapokea kwa furaha habari za kutangazwa kuwa Mwenye Heri, Papa Paulo wa VI, hapo tarehe 19 O0ktoba 2014, siku ambayo pia itakuwa ni kufungwa kwa Sinodi juu familia. Tendo hilo ni la muhimu kwani linaunganisha uwepo wa washiriki kutoka pembe zote za dunia.

Kutangazwa kwa Papa Paulo wa VI kuwa Mwenye Heri katika mantiki ya Sinodi , ni ishara ya mshikamano wa baada ya kupita miaka 50, Papa huyo aliongoza na kumaliza Mtaguso mkuu wapili vatican, na wakati wa sasa ni Papa Francesco ambaye ameitisha Mkutano Mkuu wa Sinodi ya maaskofu ikiwa ni hatua za mwanzo kwa sababu, mwaka 2015 kutakuwa na Sinodi ya kawaida ya Maaskofu,ambayo itakamilisha na kuto aujumbe wake juu ya mada hii ya familia, vilevile utakuwa ni wakati wa furaha ya kusherehekea kumbukumbu Mtaguso Mkuu wa Pili .

Aliwashukuru washiriki wa Sinodi hiyo wapatao 253 wakiwa na Papa Francesco kiongozi wa Mabaraza la Maaskofu yote ya ulimwenguni . Aliwakumbuka wote katika mikutano mikuu ya maandalizi ya sinodi hiyo. Na kutoa taarifa zote tangu kuanza kwa maandalizi ya vikao vya sinodi hadi kufikia siku ya Jumapili 5 Oktoba kwenye ufunguzi rasimi wa Sinodi maalumu.

Alitaja , kufikia hatua ya sasa, roho ya sinodi na muungano wa kidugu, vimesaidia kuandaa mkutano huo kwa kusikiliza mawazo kutoka kwa watu wa Mungu kwa njia ya maaskofu, mapadre , washamasi na walei.

Maswali yaliyotungwa kwa makini yalisambazwa kote duniani katika mabaraza ya maaskofu mapadre, waamini, mashirika ya walei, watawa. Majibu ya maswali hayo, yaliweza kuwa msaada mkubwa kwa wajumbe wa Kamati Kukuu ya maandalizi ya sinodi, kwani yalionyesha watu kuwa na roho ya wazi katika kujibu maswali hayo.







All the contents on this site are copyrighted ©.