Shirika la Kazi la Dunia ambao ni mkono wa Umoja wa Umoja wa Mataifa katika masuala
yanayohusiana na kazi na ajira duniani, Jumatatu 30 Septemba, limeadhimisha Siku
ya Kimataifa ya Wazee Wastaafu na wito wa kutoa Kipaumbele katika utoaji wa “chanjo”
ya pensheni na upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee . Guy Ryder , Mkurugenzi
Mkuu wa wa ILO, katika Siku hii ya Wazee, amesisitiza umuhimu wa kushughulikia
masuala ya idadi ya watu kupitia sera jumuishi za kukuza ajira na ulinzi wa kijamii.
Tamko kutoka ILO linasema, maisha marefu na afya nzuri, ni moja ya matokeo muhimu
zaidi katika maendeleo ya binadamu, katika kupimo cha uwezo wa binadamu katika kuboresha
maisha ya binadamu, kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa sababu hii, ongezeko
la kasi la idadi ya wazee katika nchi zote, zenye viwanda vingi na hata zile zenye
viwanda vichache, tofauti katika kasi hiyo ni ndogo. Na kwamba kufikia mwaka 2050,
inatarajiwa idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 itakuwa mara tatu zaidi,
wakati idadi ya wenye kuwa na miaka chini ya 15 itabaki kama ilivyo au bila mabadiliko
makubwa. Na kwamba, Robo tatu ya watu wazima, watakuwa katika nchi katika nchi
zenye viwanda vichache wengi wao wakiwa wanawake. ILO inasema, mabadiliko haya ya
idadi ya watu, yatakuwa na athari kubwa pia katika mabadiliko ya dunia. Ni muhimu
kuelewa hili, kama msaada kwa nchi kubadilisha sera zake juu ya maisha ya watu tangu
sasa.
Ni maelezo ya Mkurugenzi wa ILO, Bwana Guy, akirejea repoti ya mwaka
ya shirika lake. Anaendelea kusema, ili kukabiliana na changamoto hii, itakuwa muhimu
kuwa na sera jumuishi zenye kuzingatia kukuza ajira na ulinzi wa kijamii na uwezo
wa kuchochea mzunguko mzuri wa ajira, ulinzi wa kijamii na maendeleo. Baadhi ya nchi
zimeonyesha kuwa macho juu ya sera za haki na ufanisi wa nafasi kwa ajili ya watu
wazee. Ametaja sera hizo kuwa ni mchanganyiko wa sera, katika utambuzi wa umuhimu
wa kutegemeana katika mabadiliko ya idadi ya watu, ajira, ulinzi wa kijamii, uhamiaji,
kazi na maendeleo ya kiuchumi. Ni kukutana na changamoto za mazingira mpya ya idadi
ya watu iliyoundwa na idadi ya watu wazee , majadiliano ya kijamii, yanakuwa ni muhimu
kutambua majibu yanayo faa zaidi, kwa ajili ya ufanisi, usawa na ustawi endelevu.
Mkuu wa ILO, pia alitoa wito wa kuhakikisha wazee wanapata pensheni ya kutosha
na huduma nzuri za afya, kama msingi umoja na mshikamano wa jamii, katika kuthamini
utu wa mtu bila kujali umri. Kwa kutambua umuhimu wa usalama mapato katika umri wa
mkubwa, katika nchi nyingi za kipato cha juu na pia katika baadhi ya mataifa yenye
kipato cha kati, kipato cha pensheni kimepanuliwa vizuri kwa wazee. Lakini kwa nchi
nyingi zenye kipato cha chini, malipo ya pensheni na huduma za afya kwa wastaafu na
wazee kwa ujumla vipo katika hali za kusikitisha, hasa ikiathiriwa zaidi na ongezeko
la kasi la Idadi ya watu. Hivyo basi upanuzi wa pensheni, na upatikanaji wa huduma
za afya kwa wazee ni kipaumbele kwa ajili ya kila mtu. Adhimisho la mwaka huu la
Siku ya Kimataifa ya wazee, ILO ilizindua ripoti “Hifadhi ya Jamii kwa Watu Wazee:
mwenendo muhimu wa sera na takwimu”, ambayo ina uchambuzi wa kina juu ya mada hii
ni muhimu sana hasa kwa wanawake wazee . Karibu nusu ya watu wazee katika ulimwengu
hawana pensheni. Kwa mujibu wa ripoti ILO, asilimia 52 ya wazee hupokea pensheni,
lakini kwa viwango duni na hali imekuwa mbaya zaidi kama matokeo ya ukali wa kipeo
cha uchumi duniani.