2014-10-03 16:26:40

Papa asema, binadamu ana tatizo la kumwekea Mungu masharti


Papa Francisko katika Homilia yake Ijumaa 3Octoba katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican amesema kwamba ,hamu ya Mungu ni kukoa binadamu, lakini tatizo ni kwamba, binadamu mara nyingi, hulazimisha sheria zake mwenyewe kwa wokovu wake.Ukaidi huo wa binadamu umejitokeza katika maandishi mengi ya Biblia hadi kilele cha maisha ya Kristo hapa duniani.

Papa Francisco alieleza hili kwa kuitafakari Injli ya siku ambamo Yesu alionyesha huzuni juu ya watu wake walio mgeuzia kisogo kama neno lake lisemalo “ kama Tiro na Sidoni wangepata miujiza ambayo imefanyika miongoni mwenu, na Yesu kutoa onyo juu ya Korazin na Betsaida, kwa muda ule wangekuwa wameshaokoka.

Papa anaongeza kwamba, katika historia ya wokovu inaonyesha kama vile walivyowakataa Manabii na kuwaua kabla yake, kwa sababu walionekana kubugudhi watu, na sasa walifanya kitendo hicho kwa Yesu.
Na hizi ni vurugu za upinzani dhidi ya waliokolewa zilizo sababishwa na viongozi wa watu. Aliongeza.

Ni wale wale watawala wanaofunga milango ambamo Mungu anapenda kuwaokoa. Na kwa namna hiyo walitambua mazungumzo ya Yesu yenye nguvu kwa watawala wa nyakati hizo wanaopigana, na kumweka katika majaribu, wanamwekea mtego kuona kama ataanguka, kwa sababu ni mpinzani dhidi ya waliokolewa. Lakini Yesu anawaeleza kwamba yeye anawajua , maana wao ni kama vile watoto walio pigiwa filimbi lakini hawakucheza,waliimbiwa maombolezo , lakini hawakulia, Je wanataka nini? Papa alijibu kwamba wanataka kufanya njia zao za wokovu, kwamba hiyo ndi ndiyo njia ya kumfungia Mungu milango.

Alimalizia akisema kwamba, Yeye anaamini kwamba Yesu ni Mwalimu mwenye kufundisha njia ya wokovu.








All the contents on this site are copyrighted ©.