Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Haki na Amani
Jumatano 1 -3 Octoba ulianza mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki
na Amani, kwa lengo la kujadili Waraka wa Kitume wa Papa juu ya Furaha ya Injili
(Evangelii Gaudium ) ambapo Papa Francisco alifunga nao mwaka imani. Waraka huu umeleta
hamasa mpya katika shughuli za Baraza la kipapa la haki na amani. Pamoja na mada
muhimu kwa shughuli za Baraza la kipapa la Haki na amani na shughuli za jamii katika
nchi zilizo na hali za ghasia na migogoro, wawakilishi wa nchi hizo wataHudhuria
mkutano huo wa mwaka. Vilevile watagusia mada ya maadhimisho ya miaka 5 ya Waraka
wa (Caritas in veritate) na maadhimisho ya miaka 10 ya maandishi ya Mafundisho ya
kanisa. Taarifa inasema kwamba watatafakari pia Waraka wa Upendo katika Ukweli
"Caritas in veritate" na maandishi ya mafundisho ya kanisa, na uwezekano wa kusahihisha
au kuboresha Tarehe hiyo ya mkutano imependekezwa kwa lengo la kuwawezesha wajumbe
husika kuhudhuria hata wale watakao hudhuria Sinodi maalumu juu changamoto ya familia
katika mazingira ya uinjilishaji, itakayoanza tarehe 5-19 Octoba Mkutano wa Balozi
wa Papa katika nchi za Mashariki ya Kati na Viongozi wa Idara za Curia ya Roma.