2014-10-02 08:31:59

Karama ni kwa manufaa ya wote


Katika kuendeleza katekesi yake juu ya karama za kanisa , Jumatano Papa Francisko kwenye uwanja wa Vatikan amendelea na mafundisho juu ya Karama za Kanisa, ya kwamba, tangu mwanzo kanisa , Bwana ametoa zawadi ya Roho Mtakatifu ziweze kuimarisha Kanisa.

Na kati ya zawadi hizo kuna nyingine ambazo zinaonekana kuwa muhimu ambazo zinajenga Jumuiya ya kikristo katika safari yake. Zawadi hizo ni karama . Je karama ni kitu gani, je tunaweza kuzipokea namna gani kwani ndani ya kanisa kuna aina nyingi za karama na zinapaswa kuoneka kwa mtazamo mzuri wa kujiuliza.

Papa alisema kwamba katika lugha ya wote neno karama inasikika , ikiwa na maana ya talanta , uwezo asilia wa binadamu. Kwa mfano ya watu mbalimbali wakiwa na uwezo wa kufundisha au kufanya jambo fulani, utasikia wanasema hawa wana karama,au ni bora lakini karama maaana yake ni nini?

Kwa upande wa ukristo, karama ni jambo kuu zaidi ya sifa ya mtu aliyo nayo. Karama ni neema , ni zawadi kutoka kwa Mungu baba, kwa njia ya Roho mtakatifu. Ni zawadi ambayo inatolewa siyo kwaajili ya sifa binafsi uliyo nayo au kuwa na akili zaidi ya wengine ni kwasababu unastahili. Ni zawadi ambayo Mungu anatoa bure, na kwa upendo ule ule ili upate kufanya huduma katika jumuiya kwanza kwa mafao ya wote.

Papa aliongeza kwamba Mungu anatoa karama kwa mtu si kwa ajili yake binafsi bali ni kwa ajili huduma ya jumuiya nzima. Baba Mtakatifu kabla ya kwenda kutoa katekesi, alikutana na kundi la watoto walemavu na wahudumu wao kwenye ukumbi wa Paulo wa VI , watoto hawa walisindikizwa na chama kinachojishughulisha na watoto hao, je chama hicho, watu hao ni wakina nani? Hiyo ndiyo karama ya kutibu watoto walemavu,aliongeza Papa.

Alizidi kufafanua juu ya karama kwamba ieleweke siyo rahisi mtu binafsi kujitambua karama aliyo nayo , akitoa mfano, wengine husikika wakisema mimi sina uwezo wa kufanya hili, na kuna wengine wenye kujigamba kuwa na uwezo wa kufanya jambo kumbe siyo, kama vile kuna wanaojigamba kuwa waimbaji wazuri na kumbe siyo, hakuna anayemnyamazisha kusema kwamba nyamaza kwani unapoimba unaleta vurugu. Na bahati mbaya wengi hawawezi kuwakosoa watu hawa wenye kujigamba wenyewe. Ndani ya jumuia inayoanza kukua na kuchanua, huchanua zawadi kutoka kwa Mungu , na ndani ya jumuiya ni vizuri kujifunza kuzitambua kama ishara za upendo kwa watoto wake.

Na hivyo kila mmoja ni bora kujiuliza swali , je kuna karama yoyote ambayo Bwana amenijalia, kwa njia ya Roho Mtakatifu na kwa ndugu na jumuiya ya wakristo?

Je ni mwenendo gani nilio nao juu ya zawadi hiyo?, naishi kwa ukarimu, nikitoa huduma kwa ajili ya wote , au nimeachilia mbali na kijisahu , au kwa sababu ya karama hiyo inanifanya kuwa na kiburi cha kuweza kuwalalamika na kuwataka wengine wafanye kama wewe.

Papa aliendelea katika mafundisho yake kwamba hayo ni maswali ambayo kila mmoja anapaswa kujiuliza iwapo unayo karama na karama hiyo inajulikana na kanisa ,Vilevile ninaifurahia karama hiyo na kuridhika nayo,, au nina wivu kidogo na karama za wengine na ninapenda niwe nazo karama zao. Papa anakumbusha kwamba karama hatuzitengenezi sisi wenyewe bali ni zawadi kutoka kwa Mungu peke yake.

Papa aliendelea Mafundisho yaliendelea kwamba Uzoefu wa kufurahisha ni ule wa kugundua karama mbambali za roho wa Mugu alizo toa kwa kanisa . Na karama hizi zisiwe ni kikwazo na kuleta mvurugano , bali zote hizo ni zawadi ambazo Mungu anazawadia Jumuiya ya kikristo, ili ipate kukua kwa upendo mshimano, imanii ya upendo wake , ni kama mwili mmoja na mwili wa Kristo.

Roho hiyo ndiyo inayotoa karama mbalimbali na kufanya umoja wa kanisa: Kutokana na wingi wa karama hizi, mioyo ifunguke kwa furaha na kufikiria , Ni jambo zuri! Ni zawadi nyingi kwasababu sisi wote ni watoto wa Mungu na tumependwa kwa namana ya pekee.

Baba Mtakatifu alimalizia katekesi yake akikumbuka kwamba kanisa linafanya kumbukumbu ya Mtakatifu Tereza wa Mtoto Yesu, aliyekufa akiwa na umri wa miaka 24 tu alipenda sana kanisa , na alitaka awe mmisionari , lakini alitaka awe na karama zote na kusema mimi nataka kufanya ili na lile… , lakini wakati wa sala zake alijisikia rohoni mwake karama yake ni upendo, na katika maneno yake alisema neno moja zuri kwamba “katika moyo wa kanisa mimi nitakuwa upendo.

Papa alibainisha kwamba kila mmoja anayo karama hii , uwezo wa kupenda . Aliwataka watu wote kumuombe Mtakatifu Teresa wa mtoto Yesu uwezo wa kupenda sana Kanisa , na kukubali kwa upendo karama za watoto wa kanisa na Mama Mtakatifu wa kanisa.








All the contents on this site are copyrighted ©.