2014-10-01 08:50:30

Kard. Baldisseri ahimiza kuiishi njia ya mapinduzi ya digital


(Radio Vatican) "Mawasiliano Jamii ni msingi wa Kanisa ambao unastahili kukuzwa na kuimarisha", ni maneno ya Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya familia, wakati wa kuadhimisha Misa ndani ya Kanisa dogo la Radio vatican, kama sehemu ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Malaika Mkuu Gabrieli, msimamizi wa Redio Vatican.

"Safiri na kuishi njia ya digital, katika ulimwengu wa sasa, na muwe kama malaika ambao utume wao daima ni kupeleka ujumbe wa Mungu. Kumbukeni kwamba shughuli zenu za mawasiliano ndani ya Redio Vatican ni kumwakilisha Papa. Ni kufikisha ujumbe wa Papa katika kila kona mabako Redio Vatican inasikika". Kardinali Baldisseri aliendelea kuwakumbusha wafanyakazi wa Redio Vatican kwamba, Papa Francesco mara baada ya kuchaguliwa alikutana na wanahabari na kuwaeleza kwamba nafasi yao ina sura mbili ya taaluma, kama wanahabari na kama watangazaji wa Injili. Na kwamba kazi yao hii, inahitaji utafiti, usikivu na uzoefu vile viile, na mara nyingi, inapaswa ifanyike ki ukweli, kwa wema na uzuri.Hiyo inawafanya kuwa karibu na kanisa kwa kuwa kanisa lipo kwa ajili ya kutangaza ukweli, wema na uzuri wa mtu ambaye ni Kristo.

Kardinali alikumbusha tena kwamba Papa Francisco alisema ”kazi hiyo inapaswa kuonekana wazi kwani wote tumeitwa siyo kujitangaza sisi wenyewe, bali ni kuzingatia vipengere hivi vitatu ukweli, wema na uzuri ”.

Kanisa linalotangaza ujumbe wa Kristo kwa upande mwingine h utangaza ujumbe kamili wa Mungu Baba, Kardinali Baldisseri alisema akitoa mfano wa maneno kutoka katika Utume wa Kuokoa ”Redemptoris Missio” juu ya maadili, njia mpya za kuwasiliana , lugha mpya na pia mbinu mpya ya kisaikolojia.

Aliongeza kwamba, uwezekano wa kuwasiliana katika njia mpya umesambaa, ni vyema kwa binadamu wote kuzijua njia hizo. Lakini zinapaswa kukuzwa na kulindwa kwa mujibu wa maadili ya vyombo vya habari. Kadri nguvu za vyombo vya habari zinavyozidi kuongezeka, na ndivyo lazima ziwe na dhamiri ya kimaadili kwa wale ambao wanatumia njia hiyo na kwa maisha ya wale ambao wanafaidika. Kwahiyo ni lazima mawasiliano ya kijamii yawepo na kuendelezwa kama sehemu muhimu na msingi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya binadamu na Kanisa.

Karidinali Baldisseri aliyekuwa ameanza homilia yake akishukuru utume wa Radio Vatikan aliwataka wafanyakazi wake wafanye mawasiliano kulingana na ukweli,heshima , uhuru na haki. Aliwaomba wapokee wito wa maendeleo endelevu ya digital, katika dunia ya kisasa kwa misingi ya ukweli na upendo , wa kumpeleka Kristo katika moyo wa ulimwengu.

Na baada ya misa walijumuika wafanyakazi wote kwa pamoja katika fursa ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa mwaka kama ilivyo utaratibu wa Redio Vatican katika maadhmisho ya Siku Kuu ya Malaika Mkuu. Kwa mwaka huu waliopokea tuzo ni Sr Lidia Korotkova, wa Kitengo cha Ukraina, ambaye yupo Redio Vatican Tangu 1981, Profesa Silvonei Protz, Kitengo cha Brazil yupo Redio vatican tangu 1990 na Giuseppe Fantucci anayehusika na Kitengo cha Antena katika Kituo Kikuu cha Mawasiliano cha Redio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.