2014-09-30 08:25:18

Kanisa -uvumilivu zero kwa wanaodhulumu watoto kijinsia


Kwa Kanisa Katoliki, kila kesi ya unyanyasaji wa kijinsia inayojitokeza, hasa kwa watoto na vijana, huchukuliwa kama ni dharura muhimu ya kushughulikiwa mara moja, kwa mujibu wa sheria na kanuni za kanisa. Na kwamba Kanisa kwa wakati huu limepiga hatua katika kutakatifusha Kanisa dhidi ya aibu hii , na matokeo yake yanaonekakana mbele ya macho ya watu wote. Kwa kila anayethibitishwa kufanya uhalifu huu, ameadhibiwa vikali au kuwekwa katika hali ambamo hataweza tena kutenda dhambi hii.
Naibu Katibu wa Jimbo la Papa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, ametoa maelezo hayo , akirejea kesi ya unyanyasaji mtoto kijinsia, iliyomhusu aliyekuwa Mjumbe wa Papa katika Jamuhuri ya Domenican, ambaye mara baada ya kuthibitishwa kutenda kosa hilo, alivuliwa dhamana ya Askofu na hivyo sasa ni mlei na ameshitakiwa kama raia wa kawaida. Hatua hiyo imechukuliwa maana Kanisa halina uvumilivu kwa wanaotenda dhambi hii kubwa . Ni zero uvumilivu, kwa misingi ya kanuni za kisheria na sheria ya ndani ya kanisa iliyowekwa miaka kumi iliyopita, iliyosababisha mpaka sasa kufukuzwa kwa mamia ya watumishi wa Kanisa, Maaskofu, Mapadre na wengine wanaovunja heshima ya maisha Matakatifu na yaliyowekwa wakfu.

Askofu Mkuu Becciu alieleza hili, wakati akihojiwa na Franca Giansoldati juu ya "Ujumbe ulioandikwa katika gazeti la Il Messaggero" toleo la 27 Septemba, akiirejea kesi WesoĊ‚owski, iliyotia simanzi kubwa kanisa ambayo imeshugulikiwa kwa kasi na mamlaka husika za kanisa, kama Papa Francisco alivyo agiza.
Askofu Mkuu anaendelea kusema kwamba, mapambano dhidi ya madhulumu ya kinjisia hasa kwa watoto na vijana ni mapambano dhidi ya dhambi kubwa, dhidi ya uovu mkuu, na hivyo amehimiza vyombo vyote vya usalama na ulinzi wa raia walitazame kwa makini suala hili na unyanyasaji katika jamii ya leo, ambayo imepiga hatua kubwa katika mawasiliano ya mtandao wa kimataifa wa picha za aibu za watoto katika ngazi zote, kitaifa , kimataifa na ngazi za chini kwenye matawi yake. Kukomesha mtandao huo kunaweza saidia ukomeshaji wa biashara na starehe zinazo fanywa na wafanya biashara hao dhalimu, wanaoweka fedha chafu mbele kama msingi wa maisha yao.
Amesema, hakuna kuwaonea aibu wahalifu hao. Huu ni wakati wa kuwataja hadharani na kuwaweka wazi hata kati safi za mitandao na maoni. Ni suala la kuunganisha nguvu na mshkamano wa wote, Kanisa na jamii kwa ujumla katika kupambana na uovu huu,kwa lengo la kulinda watoto, na hata pia watoto katika nchi maskini, wanaoingizwa katika biashara haramu na aibu ya utalii wa ngono .
Na kwamba, mapambano dhidi ya unyanyasaji wa watoto, yanaweza kufanikishwa zaidi kwa kutumia silaha ya elimu katika hatua zote za makuzi namajiundo ya watoto na jamii, tangu ndani ya familia, mashuleni na katika uwanja wa michezo. Inahitaji juhudi za pamoja katika matukio yote ya kijamii, kutokana na sera na taasisi wale wanaohusika na utoaji wa elimu na mafunzo. Na kutokana na ujinga huu kuongezeka katika utamaduni wa leo, kunahitajika hatua kali za kisheria kupambana na mawazo ya vurugu na kulazimisha kwa watoto kuingia katika dhambi hii. Kwa upande wake, Kanisa linatoa kipaumbele cha juu sana, hasa katika miundo yake Malezi na kichungaji.








All the contents on this site are copyrighted ©.