Mkutano Mkuu wa 59 wa Umoja wa Mataifa unatazamiwa kufungulia 23Septemba mjini New
York , unahudhuriwa na viongozi Wakuu wa nchi na Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za
dunia. Mkutano huo unahusu mabadiliko ya hali ya hewa.
Viongozi Wakuu wa madhehebu
ya dini wametoa tamko litakalowasilishwa katika mkutano huo, likiwa na kaulimbiu:"
hali ya hewa, Imani na Matumaini: Muungano wa tamaduni za dini juu ya umoja endelevu”.
Tamko
hilo limesainiwa na viongozi wakuu wa madhehebu mbalimbali na kati ya viongozi hao
30, yupo Kardianali John Onaiyekani wa Abuja Nigeria, Kardinali Oscar Rodrigue Maradiaga
wa Caritas Internationalis, Padre Michael Czerny S.J mwakilishi wa Baraza la Kipapa
katika Tume ya Ushauri, haki na Amani.
Tamko hiili linasema kwamba Viongozi
wawakilishi wa madhehebu mbalimbali ya dini wamekusanyika pamoja kuonyesha mshikamano
wao pia wasiwasi walio unao kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo inaathiri
ardhi ambayo mwanadamu amekabidhiwa aitunze.
Wanatambua kutokana na taarifa
za kisayansi juu ya ukosefu na hatua madhubuti kuchukuliwa dhidi ya kukomesha mabadiliko
ya tabia nchi. Kitendo hicho cha kutokuchukua hatua zinazostahili zinazidi kusababisha
mabadiliko haya , na hivyo viongozi hawa wako tayari kufanya majadiliano na wanahusika
na wale wasiotaka kutokujali suala hili.
Kutokana na vyombo vya habari , mitandao
ya kijamii ,jumuiya na jamii zote zinaona mabadiliko haya ya tabianchi kila pembe
ya dunia. Ndugu wote katika dunia hii wamesikika wakiongea athari mbaya zinaowagusa
watu na hali ya nchi.
Na athari hizi zinajitokeza katika maeneo mbalimbali
na hasa kwa wale wanyonge wanao dhulumiwa haki, watu masikini. Inapojitokeza matatizo
au maafa katika maeneo ya wale wanaosababisha, ndipo huonekana dharura ya haraka katika
haja ya kuwa na mabadiliko katika utendaji.
Tamko hili lasema, mabadiliko
ya tabianchi ni mojawapo ya kikwazo cha maendeleo na huendeleza umasikini kwani matukio
ya hali ya hewa yanasababisha njaa, maafa, kuyumba kwa uchumi, kulazimisha watu kuhama
na kuzuia maendeleao endelevu.
Kipeo cha tabianchi kinahusu binadamu wote
katika sayari hii ya dunia, Na hivyo inakuwa ni wajibu wa binadamu wote, kutathimini
na kupata ufumbuzi wa haraka . Pamoja na hayo viongozi wa muungano wa madhehebu wanasema
wako pamoja kutoa mchango wa kupunguza maafa yanayojitokeza, kama vile, kupunguza
hewa ya ukaa ,kutoa elimu juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, vilevile kuzuia matumizi
mabaya ya mafuta.
Kwa Imani zao za kiroho na katika matumaini endelevu,
watajitahidi ,kuchochea dhamiri binafsi na kuwatia moyo wenzao wote katika shughuli
za kitume na jumuiya zote kufikiria hatua hizo kwa haraka.
Vilevile wanasema
wanao uhakika kwamba suala linalohusu Tabianchi kamwe haliwezi kufanyika katika nchi
moja , bali kwa ushirikiano wa Jumuiya zote za mataifa ,na hasa misingi ya kuaminiana,
haki, na usawa, tahadhari, kurithisha kizazi na majukumu ya pamoja.
Wanatoa
wito na kuhamasisha nchi tajiri kusaidia nchi zilizo masikini, ili nchi zote duniani
na hasa katika nchi zinazopiga hatua za maendeleo kama vile mataifa yaliyoko Kusini
mwa Jangwa la sahara ,wajitoe kwa ukarimu kusaidia ili nchi hizo zipate nguvu katika
ufundi na teknolojia
Vilevile Wanawatia moyo viongozi wakuu wa mataifa , mawaziri
wakuu kutoa hadi za kuchangia mifuko ya vyombo vina shughulikia na kupambana na uharibifu
wa tabianchi, bila kusahau kwamba viongozi hao wakubaliane kuweka mikakati ya kuzuia
ongezeko la joto la dunia lisizidi nyuzijoto 2.