2014-09-16 14:53:00

Mkutano wa Makadinali washauri wa Papa Francisko


(Vatican Radio) Mkutano wa sita wa Baraza la Makardinali 9 na Papa Francisco, ulianza Jumatatu asubuhi katika Jengo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican, na unaendelea hadi Jumatano 17 Septemba 2014.
Baraza la Makardinali 9, ambalo pia linajulikana kama Baraza la wajumbe tisa, wajumbe wake waliteuliwa na Papa Francisco 13 April 2013 ikiwa umepita mwezi mmoja tangu alipochaguliwa kuwa Papa. Na 28 Septemba 2013, aliwathibitisha katika jukumu la kuwa washauri wa Papa, kwa ajili ya utawala wa Kanisa zima la ulimwengu na katika masuala yanayohitaji uandaaji wa mpango kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya kitume ya "Mchungaji Mwema”, kwa Idara za Curia ya Roma.

Tangu kutajwa Baraza mwaka jana lilifanya vikao vyake viwili Oktoba 1-3, 03-05 Desemba, 2013. Kwa mwaka huu limefanya vikao vinne , Februari, April , Julai , na Septemba
Makardinali Wajumbe wa Baraza ni Kardinali , Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Jiji la Vatican , Kardinali , Askofu Mkuu Mstaafu wa Santigo de Chile, Kardinali , AskofuMkuu wa Bombay. Kardinali , Askofu Mkuu wa Munich. Kardinali , Askofu Mkuu wa Kinshasa. Kardinali OFM Cap, Askofu Mkuu wa Boston, Kardinali , Mkuu wa Kardinali SDB, Arskofu Mkuu wa Tegucigalpa, Kardinali , Katibu wa Jimbo la Papa na Vatican.
Mratibu wa Baraza hili ni Kardinali Rodríguez Maradiaga na Katibu wa Baraza ni Askofu , Askofu wa Albano.








All the contents on this site are copyrighted ©.