2014-09-16 15:09:07

Homilia ya Papa: Bwana Anatembelea watu wake.


Unaweza kuhubiri vizuri, lakini kama haupo karibu na watu, kama uteseki na watu na uwapi matumaini , mahubiri hayo hayasaidii, ni ubatili.

Haya ni maneno ambayo Papa Francisco amesema asubuhi ya Jumanne 16Sept katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini vatican, ambamo Kanisa lilikuwa linawakumbuka watakatifu Papa Cornelius na Askofu Cipriani mfiadini.

Papa alisema Injili inasema watu wengi walikuwa wakimsindikiza mtoto aliyekufa wa mama Mjane wa Naim , Bwana akatenda miujiza yake ya kumrudishia uhai kijana. Lakini anafanya la zaidi maana yeye yuko karibu, kwani Mungu anasema kwamba aliwatembelea watu wake.,”Mungu anapofanya matembezi “kunatokea jambo kuu zaidi , kuna jambo jipya””maana yake ni kwamba uwepo wake ni muhimu na uko pale” Yesu yuko karibu.

Aliendelea Mungu alikuwa karibu na watu, yupo karibu na anaweza kutambua mioyo ya watu wote.Aliona umati na Bwana akawakaribia , Mungu anatembelea watu wake, yuko katikati yao . Ukaribu, ni njia anayoitumia Mungu.

Papa anaongeza kuna neno linalotumia mara nyingi katika Biblia ,” Bwana alishikwa na huruma”. Ni huruma ile ile inayojitokeza katika injili alipokuwa amewaona watu wengi kama wasiokuwa na mchungaji.

Mungu anapotembelea watu wake , yeye yu karibu nao, anajisikia kuwa mwenye huruma: anashikwa simanzi. Bwana anawatembelea watu wake kwa Ukaribu na huruma.

Iwapo tunataka kupeleka Injili ya neno la Yesu, barabara yake ni ukaribu na uhuruma.

Kuna njia nyingine ya waalimu waliokuwa wakuhubiri zamani za kale, yaani walimu wa sheria , waandishi na wafarisayo, wao walikuwa wanaongea wakiwa mbali na watu.

Walikuwa wakiongea vizuri, wakifundisha vizuri sheria, lakini walikuwa mbali na watu. Lakini hii haikuwa ni matembezi ya Bwana , ilikuwa ni kitu kingine. Watu hawakupokea mafundisho hayo kama neema kwasababu walikuwa wanakosa hali ya ukaribu, walikosa huruma na kuteseka nao.

Papa aliongeza kwamba kuna neno jingine , Bwana anapotembelea watu wake, “yule aliyekufa anapata kukaa , na kuanza kuongea, na Yesu anamkabidhi kwa mama yake”.

Bwana anapowatembela watu wake, anawarudishia matumaini daima.

Unaweza kuhubiri neno la Mungu kwa mshangao mkubwa, kwani katika hitoria wamekuwepo wahubiri wazuri, lakini kama wahubiri hawa hakuweza kupanda mbegu ya matumaini , mahubiri hayo hayasaidii kitu ni ubatili

Papa alimazia akisema kuwa kwa kuangalia Yesu anayemrudishia mtoto mzima kwa mama yake , tunaweza kutambua namna gani Mungu anatembelea watu wake.

Na inatupasa kuomba neema ya kwamba ushuhuda wetu katika ukristu uwe ni ushuhuda wa kupeleka matembezi ya Mungu kwa watu wake, maana yeke kuwa karibu na watu na kupanda mbegu ya matumaini kwa watu wake.








All the contents on this site are copyrighted ©.